0

Chadema Noma sana!! WAWEKA HISTORIA SHINYANGA VIJIJINI, MBOWE SASA NI CHIFU WA WASUKUMA

Hapa ni katika katika kata ya Iselamagazi wilayani Shinyanga (jimbo la Solwa wilaya ya Shinyanga vijijini) kwenye mkutano wa hadhara, ambapo jana
mwenyekiti wa Chama Cha demokrasia na maendeleo taifa (CHADEMA), Freeman Mbowe alisimikwa kuwa chifu wa Kisukuma na wazee wa kimila wa kabila la Kisukuma,kutokana na  chama hicho kuonekana kuwa mstari wa mbele katika kupigania maslahi ya wananchi-Picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog

 
Wazee hao walisema wameamua kumsimika mwenyekiti huyo wa Chadema taifa kuwa Chifu wa Kisukuma, kutokana na Chama anacho kiongoza kimekuwa mhimili mkubwa wa kupigania maslahi ya wananchi katika kuhakikisha wanapata haki zao za msingi katika nyanja zote-Picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog

Naye mwenyekiti huyo wa Chadema taifa ambaye pia  ni Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe aliwashukuru wazee hao wa kabila la wasukuma kumsimika kuwa Chifu wao, huku akiudhihirishia umma kuwa Chadema siyo chama cha ukabila wala udini-Picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog

Wazee wa Kisukuma wakifanya yao katika mkutano wa hadhara wa mheshimiwa Mbowe ambapo maelfu ya watu walishuhudia tukio hilo-Picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog

  

Mbowe alisema hiyo ni historia katika nchi hii na kuonyesha kwamba Chadema hakina ubaguzi bali ni chama cha wananchi wote, chenye lengo la kuleta ukombozi wa nchi , ambao ulipotea zaidi ya miaka 50, hivyo wanaodai Chadema ni Chama cha ukabila waache lugha hizo za upotoshaji-Picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog

Awali Makamanda wa CHADEMA wakiwasili eneo la tukio-Picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog



Post a Comment

HOME

 
Top