0
HUYU NDO EDWARD MORINGE SOKOINE SHUJAA WA WANYONGEMZALENDO WA TANGANYIKA,ADUI WA WAHUJUMU UCHUMI NA WATENDAJI WAZEMBE1/8/1938 -12/4/1984

"Ole wao wale wanaotumia nafasi zao za umma na serikali,kuiba,kuhujumu uchumi,kupokea rushwa,maana salama yao ni kudra za Mwenyezi Mungu labda nisiwajue"

Hayo ni maneno aliyowahi kuyatamka hayati kaka na mzalendo wa taifa hili shujaa Moringe Sokoine,wakati akilihutubia kwenye mkutano kikao cha NEC mjini Dodoma 12/04/1984,takribani miaka 30 iliyopita,wakati huo vita ya kupambana na suala la uzembe makazini,ulangunguzi,rushwa na biashara ya magendo,enzi hizo taifa lilikuwa la moto kila sehemu ilikuwa moto,lakini mpaka leo kauli yake inaishi,inatumika,inaamsha hali ya uzalendo na maadili ya taifa hasa wakati huu ambapo wanasiasa na serikali kwa ujumla wanaishi kinyume na misingi mikuu ya taifa hili,misingi mikuu ya chama chao na msingi mkuu wa uwajibikaji wa serikali,leo tunamkumbuka,tunakumbuka kifo cha mpendwa wetu huyo kwa yale mazuri aliyoifanyia Tanganyika kwa ujumla wake,lakini pindi tunakumbuka kumbukumbu hii tujiulize je?utakapofariki utakumbukwa kwa lipi?je viongozi wetu wanaishi kimatendo kma hayati wetu Sokoine?

ALIPOTOKA MH SOKOINE NA SAFARI YAKE NDEFU KUELEKEA KULETA TANGANYIKA TUITAKAYO.

Hayati Sokoine alizaliwa mnamo mwaka 1/8/1938 katika wilaya ya MAASAI LAND ambayo kwa sasa inafahamika kama wilaya ya Monduli,wilaya iliyoko mkoani Arusha,hayati Sokoine alipata elimu yake ya msingi Monduli,akafaulu kujiunga na shule ya sekondari Umbwe,hii ilikuwa ni kuanzia mwaka 1948 mpaka 1958,alipomaliza hapo alijiunga rasmi na chama cha TANU 1961,kisha alipata nafasi ya kwenda nchini Ujerumani mwaka 1962 mpaka 1963 kusomea mambo ya uongozi na utawala na aliporudi akateuliwa kuwa afisa mtendaji wilaya ya Maasai Land,na kutiokana na ufanyakazi wake uliotukuka wilayani Monduli wananchi hawakuwa na budi kumchagua kuwa mwakilishi wao bungeni yaani mbunge wa Monduli na ufanisi wake kiutendaji ulionekana machoni mwa watendaji wakuu wa serikali na hayati baba wa taifa Nyerere na akachaguliwa kuwa Naibu wa wizara ya mawasiliano na Usafiri hii ilikuwa mwaka 1967,kama hiyo haitoshi nyota ya kiuongozi ilizidi kumwangazia ambapo mwaka 1972 aliteuliwa kuwa waziri wa Usalama na hatimaye mwaka 1977 aliteuliwa rasmi kuwa waziri mukuu wa iliyokuwa serikali ya Tanganyika,na Muungano wa Tanzania,

Hayati sokoine alikuwa hasa mzalendo na aliependa siasa za ujamaa na hata kupelekea kumwomba baba wa taifa ruhusa ya kusisimama kwa mda kama waziri mkuu ili aende kusomea zaidi mambo ya ujamaa nchi za nje,hii ilikuwa mwaka 1981,1983 alirudi kuendelea kama waziri mkuu kuanzia wa Tanzania mpaka siku ya tarehe 12/4/1984 alipopata ajali mbaya ya kugongwa na gari lililokuwa likiendeshwa na mkimbizi wa kisiasa kutoka nchini Afrika kusini aliyejulikana zaidi kwa jina la Dube,eneo la Wami Dakawa sasa Wami Sokoine mkoani Mororgoro,ajali iliyopelekea mauti yake palepale,kifo ambacho mpaka leo kinaacha maswali mengi na kwa bahati mbaya hakuna hata mwandishi mmoja aliefanya mahojiano na bwana Dube ambaye kwa sasa yupo nchini Afrika kusini anakula bata,,

UTATA WA KIFO CHAKE NA MASWALI MAGUMU YASIYOJIBIKA KIRAHISI

Itakumbukwa kwamba karibia viongozi wakubwa wote wa serikali waliondoka mjini Dodoma kwa ndege mara baada ya kikao cha NEC,Isipokuwa hayati Sokoine ,yeye alisema wazi ni muumini wa sera ya kilimo ni uti wa mgongo wa taifa,hivyo alipendekeza kusafiri kwa njia ya barabara ili ajionee Mashamba makubwa na maendeleo ya kilimo kwa ujumla,

2:Gari lililomgonga liliwezaje kupenya magari yote yaliyokuwa kwenye msafara wa waziri mkuu Sokoine mpaka kulifikia gari la marehemu Sokoine na kuligonga?vp trafiki walikuwa wapi mpaka lori hilo limfikie kiongozi huyo?vipi maafisa wa ulinzi ambao kazi yao ni kumlinda?

3:Katika ajali hiyo aliyefariki ni hayati Sokoine pekee,vpi kuhusu wengine kwani hakuna hata aliyejeruhiwa pakubwa

4:Aliyesababisha ajali hiyo alikuja kuachiwa huru na akarudishwa kwao A,kusini,

TETESI JUU YA UTATA WA KIFO CHAKE

Ni ukweli kwamba ukiwa kiongozi unaetimiza majukumu yako kikamilifu ni lazima utakuwa na maadui wengi na wanaokutafta kwa kila namna,hayati sokoine kutokana na vita yake dhidi ya Wahujumu uchumi,mtakumbuka wakati wa vita hiyo kuna watu walienda kuficha bidhaa mapolini na wengine kumwaga mitoni,baharini na ziwani,hali ilikuwa tete kwa wahujumu uchumi pia Walanguzi,wazee wa Magendo,wala rushwa na watendaji wazembe wa serikilini,na hapa anatajwa mzee Kawawa kuwa alikuwa miongoni mwa watu waliokemewa na maremu wakati wa kikao hicho cha mwisho mjini Dodoma,
Pia inadaiwa aliiva katika misingi ya kijamaa kupita kiasi,hali ambayo ilimtisha hata baba wa taifa
Je ni ajali ya kawaida iliyotokana na mikono na mapenzi ya Mungu?ama mkono wa binadamu?swali hili ni gumu na lina dead end

MCHANGO WAKE KWA TAIFA NA MISIMAMO NA MITAZAMO YAKE

1:Aliamini katika Haki,Usawa na uwajibikaji
2:Aliamini katika siasa za ujamaa zaidi ya siasa yeyote ile.
3:Aliamini kwamba maendeleo huja kwa watu kujituma kufanya kazi halali na bidii.
4:Aliamini katika mabadiliko chanya
5:Alikuwa mzalendo hasa kwa taifa hili
6:Aliichukia vitendo vya rushwa,hujuma,uhujumu uchumi,ulanguzi na magendo.
7:Alikuwa mtu wa vitendo na kamwe alikuwa si mtu wa kupenda kulalamikalalamika.

MCHANGO WAKE KITAIFA

1:Alikuwa mstari wa mbele enzi za vita ya Kagera pindi tunampiga Nduli Idd Amini.
2:Alianzisha vita dhidi ya uhujumu uchumi,biashara ya Ulanguzi,Magendo na aliichukia Rushwa kwa vitendo
3:Alikuwa mzalendo wa kweli wa taifa hili.
4:Aliamni katika siasa na kilimo,akiamini kilimo ni uti wa mgongo wa taifa hii ilipelekea kutotaka kupanda ndege ili ashuhudie juhudi kubwa za Watanganyika katika suala la kilimo
5:Alitunza na kutukuza tamaduni za kiafrika na utaifa wa mtanzania.

Hitimisho, leo ikiwa imepita takribani miaka 30,tangu shujaa wetu na mzalendo hayati Edward Moringe Sokoine tangu atangulie mbele ya haki, je viongozi wetu wa sasa wanaishi na kutenda kwa ajili ya manufaa ya umma kama hayati Sokoine?je?Pengo lake limezibika ama bado?wito wangu kwa wanasiasa wetu nchini wasilitumie jina la kiongozi wetu huyu na baba wa taifa kwa ajili ya kunufaika kisiasa tu?wakati hawamaanishi kwani kuchagua uovu kwenye njia ya haki ni dhambi,na sikuzote ukiwa safarini huwaulizi njia wasafiri wenzako bali wale watokao huko.

(Mungu aipe pumziko la amani nafsi yake na amlaze pema peponi hayati Sokoine)
special thanx kwa

Joseph Moses OleshangayAanyor Engai Ole Lenga na Cosmas Makune

kwa msaada wa baadhi ya taarifa nilizotumia katiaka makala hii maalumu ya kumuenzi Hayati Edward Moringe Sokoine.


Default Aliyoyasema edward moringe sokoine




"Ole wake kiongozi mzembe na asiye na nidhamu nitakayemkuta: Kiongozi wa siasa hana usalama wa aina yoyote. Usalama wake ni kudra ya Mungu na Wananchi peke yake. Viongozi wazembe na wabadhirifu wahesabu siku zao. Labda tusiwajue. Hawa hatuna sababu ya kuwapa imani, kuwa tutawalinda kama vitendo vyao viovu" - Edward Moringe Sokoine, 26 Machi 1983.


"Juu ya suala hili la mapato kutolingana na matumizi ni kwamba tungependa kupunguza uongezaji wa wataalam wasiohitajika katika Serikali na katika mashirika ya umma mpaka hapo hali yetu ya uchumi itakapokuwa katika hali nzuri" - Edward Moringe Sokoine, 23 Oktoba 1982.


"Serikali inasimamia bei, lakini Serikali yetu itakwenda mpaka itasimamia bei ya mhogo, dagaa na bei ya kila kitu? Haiwezekani, vitu vingine ni lazima vizalishwe kwa wingi ili bei yenyewe iweze kujirekebisha" - Edward Moringe Sokoine, 24 Septemba 1983
"Wajibu wa kila Mtanzania, kila familia na kila anayekula ni kujilisha mwenyewe. Si wajibu wa Taifa kumlisha mtu. Unaweza ukasaidiwa unapopatikana na janga. Lakini kama hakuna janga ni wajibu wa kila mtu aweze kujitosheleza kwa chakula na atoe ziada kwa Taifa" - Edward Moringe Sokoine, 4 Oktoba 1983.


"Vijana leo wengi wana mali zaidi kuliko wazee waliofanya kazi miaka thelathini hadi arobaini. Lakini wanaitaka Serikali ndiyo iwaulize mali hiyo wameipata wapi. Hivi kwa nini mzazi asimuulize mwanae, 'mali hii umeipata wapi?'" - Edward Moringe Sokoine, 23 Oktoba 1983.


"Katika nchi inayojali haki na usawa, majeshi hayana budi yawe ni chombo cha kulinda haki na maslahi ya walio wengi. Na kamwe hayaruhusiwi kuwa ni chombo cha wachache wenye kujali nafsi zao na kusahau maslahi ya walio wengi" - Edward Moringe Sokoine, 1Februari 1977
 "Ole wake kiongozi mzembe na asiye na nidhamu nitakayemkuta kiongozi wa siasa hana usalama wa aina yoyote.usalama wake n wa kudra ya mungu na wananch pekee yake...'viongoz wazembe na waadilifu wahesabu siku zao labda tusiwajue.'hawa hatuna sababu ya kuwapa imani, kuwa tutawalinda kama vitendo vyao viovu..,..' Vijana walio wengi leo wana mali zaidi kuliko wazee waliofanya kazi miaka thelathin hadi arobain lakin wanaitaka serikal ndio iwaulize mali hiyo wameipata wapi..hv kwa nini mzazi usimuulize mwanao mali hii umeipata wap?

--------------------


Yakukumbukwa miaka 29 kifo cha Sokoine

Ilikuwa Jumatano ya Aprili 12, 1984 saa 11:30 jioni, siku ambayo Dar es Salaam ilinyesha mvua kutwa nzima. Wakati kipindi cha salaam cha Jioni Njema cha Redio Tanzania (RTD) wakati huo kikiwa hewani, mara matangazo yake yanakatishwa ghafla na wimbo wa taifa unapigwa.


Mara inasikika sauti iliyozoeleka ya Rais Nyerere wakati huo ikisema: “Ndugu wananchi, leo majira ya saa 10 jioni, ndugu yetu, kijana wetu na mwenzetu, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Edward Moringe Sokoine wakati akitoka Dodoma kuja Dar es Salaam, gari yake imepata ajali, amefariki dunia.”


Takribani miaka 29 imepita tangu kufariki kwa, Edward Moringe Sokoine, aliyepata kuwa waziri mkuu wa Tanzania katika vipindi viwili tofauti kabla ya kufariki Aprili 12, 1984.


Sokoine alikufa baada ya kutokea ajali ya gari eneo la Wami-Dakawa, wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro akiwa njiani kurejea Dar es Salaam akitokea mjini Dodoma alikokuwa akishiriki vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Kumbukumbuka kila mwaka
Aprili 12 ya kila mwaka, taifa limekuwa likiadhimisha kumbukumbu ya kiongozi huyo kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwa ni pamoja na kuendesha makongamano, midahalo, mabonanza, ibada, riadha na upandaji mlima Kilimanjaro.


Katika utawala wa hayati baba wa taifa na rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mwalimu Julius Kambarage Nyerere, katika eneo la Wami Sokoine kulijengwa nyumba moja na banda moja linalotumika kama jukwaa lakini kwa sasa majengo hayo yamechakaa, anasema msimamizi wa eneo hilo, Hamis Said Mpandachuri.


Mwananchi ilifika katika eneo hilo na kukuta mnara wa picha ya Sokoine ukiwa umepakwa rangi mpya za manjano, kijani, blue na nyeusi huku chini ya picha yake kukiwa na maneno “Alimtumikia Mungu kwa kuwatumikia watu, sauti ya watu ni sauti ya Mungu”.


Mbali ya mnara huo na majengo yaliyojengwa katika utawala wa serikali ya kwanza, pia liko jengo jipya na la kisasa ambalo linaendelea kujengwa nyuma ya majengo ya zamani. Kwa mujibu wa uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Mvomero, jengo hilo ni kwa ajili ya shule ya sekondari ya Sokoine (Sokoine memorial high school), inajengwa kama sehemu ya jitihada za wilaya hiyo za kumuenzi Sokoine.


Mbali na jitihada za halmashauri hiyo, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) ambacho pia kimebeba jina lake kimekuwa katika mikakati ya kuhakikisha kuwa kinamuenzi kiongozi huyo kwa kila hali. Kassim Msagati ni ofisa mawasiliano wa chuo hicho, anasema hayati, Edward Moringe Sokoine, alikuwa muhimili muhimu wa kuanzishwa wa chuo kikuu hicho cha kilimo ambacho ni chuo kikuu pekee cha kilimo cha Serikali nchini.


Aprili 12, 1984 bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambalo hayati Sokoine alishiriki lilipitisha sheria namba 6 ya mwaka 1984 ya kuanzishwa kwa chuo kikuu cha kilimo Morogoro. Hapo kabla chuo hicho kilikuwa ni kitivo cha kilimo cha kilimo na misitu cha chuo kikuu cha Dar es Salaam.


Kwa mujibu wa Msagati, sheria hiyo iliyopitishwa na bunge ilikiidhinisha kitivo cha kilimo cha chuo kikuu cha Dar es salaam kilichokuwa Morogoro kuwa chuo kikuu na kutaka kiitwe chuo kikuu cha kilimo Morogoro.


Lakini chuo hicho kililazimika kubadilishwa jina hata kabla ya jina la awali kuanza kutumika na kuitwa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA). Hii ilitokana na kifo cha kiongozi huyo, muda mfupi baada ya chuo hicho kuidhinishwa rasmi kwa sheria hiyo ambapo utekelezaji wake ulipaswa kuanza mwezi Julai, 1984, ndipo serikali ikakubali kiitwe Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo.




Kutokana na umuhimu huo, chuo hicho kinakila sababu ya kumuenzi Sokoine kwa vitendo na hatua hiyo imekuwa ikichukuliwa kwa kuhakikisha kila mwaka ifikapo Oktoba, chuo huandaa mdahalo maalum wa kumbukumbu ya Sokoine ambapo viongozi mbalimbali wa kitaifa hualikwa.


Historia yake
Kila kiongozi ana historia yake katika uongozi wa kisiasa, kijamii na ofisi za umma. Edward Moringe Sokoine inaelezwa alishawishiwa awe kiongozi.Kwa mujibu wa mzee Saiguran Kipuyo ambaye amekua pamoja na hayati Sokoine, ni kwamba hayati alishawishiwa kuingia kwenye uongozi.


“Kipindi kile alikuwepo Chifu mmoja akiitwa Edward Barnoti. Vijana tulimuona hatutendei haki wala kusimamia maslahi yetu hivyo tukaamua kumpenyezea mtu wa rika letu kama msaidizi wake,” anasimulia Kipuyo


Kipuyo ambaye anasema amezaliwa kati ya mwaka 1928-1944 anaeleza kuwa vijana ndio waliokwenda kumchukua Sokoine kwa nguvu kutoka kwenye shughuli zake za kuchunga eneo la Mfereji alikoenda baada ya kumaliza elimu ya msingi katika shule ya kati ya Moringe mjini Monduli.


“Tulimlazimisha kuwa msaidizi wa chifu Mkuu wa Council ya Maasai land akimsaidia Chifu Barnoti na ilipofika kipindi cha uchaguzi wa mbunge tukamlazimisha kuchukua fomu kuchuana na mzee Barnoti, tulifanya kampeni ya chini chini hadi akashinda,” anasimulia


Anasema baada ya kuchaguliwa kuwa Mbunge kwa mara ya kwanza mwaka 1965 akiwakilisha jimbo la Maasai Land inayojumuisha wilaya za sasa za Monduli, Simanjiro, Kiteto, Longido na Ngorongoro, Sokoine aliteuliwa kuwa waziri mdogo wa ujenzi kabla kuhamishiwa ulinzi na jeshi la kujenga taifa.


Tabia ya asili ya Sokoine
“Pamoja na Uwaziri Mkuu, Sokoine alikuwa yule yule. Alikuwa na tabia ya kipekee. Alikaa na kuzungumza na watu wa rika zote kuanzia wazee, akina mama, vijana na watoto, alitumia fursa hiyo kujua matatizo yao na kupata maoni kuhusu utatuzi kutoka kwa wahusika wenyewe,” anasema Kipuyo


Waliopeleka majungu kwa Sokoine walifanikiwa?
“Alipopelekewa majungu ya mtu, alimwita anayefitiniwa na kumtaka mpika majungu kusema yote mwenzake akiwepo. Kwa tabia hii alikomesha majungu,” anafafanua.


CCM na Chadema wanasemaje?
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa mahojiano maalum, Mwenyekiti wa Jumuiya ya wanawake wa CCM (UWT), wilaya ya Arumeru, Ester Maleko na Mwenyekiti wa baraza la vijana wa Chadema (Bavicha), mkoa wa Arusha, Ephata Nanyaro wanakiri Sokoine ni kiongozi aliyekuwa na tunu za kipekee aliyewahi kutokea nchini.


Hakuna kama Sokoine
Kwa upande wake, Nanyaro yeye anasema tangu uhuru, taifa halijawahi kupata kiongozi aina ya Sokoine na Nyerere ambao walipenda nchi na watu wao kwa dhati na kuwa tayari kujitolea nafsi zao kushughulikia matatizo yao.


Baadhi ya nukuu muhimu za Sokoine;
“Ole wake kiongozi mzembe na asiye na nidhamu nitakayemkuta: Kiongozi wa siasa hana usalama wa aina yoyote. Usalama wake ni kudra ya Mungu na Wananchi peke yake. Viongozi wazembe na wabadhirifu wahesabu siku zao. Labda tusiwajue. Hawa hatuna sababu ya kuwapa imani, kuwa tutawalinda kama vitendo vyao viovu” - Edward Moringe Sokoine, 26 Machi 1983


“Katika nchi inayojali haki na usawa, majeshi hayana budi yawe ni chombo cha kulinda haki na maslahi ya walio wengi. Na kamwe hayaruhusiwi kuwa ni chombo cha wachache wenye kujali nafsi zao na kusahau maslahi ya walio wengi” - Edward Moringe Sokoine, 1Februari 1977.




Niandikie,
Mathew Malunde
malundelubuyi@gmail.com,0755052883,0785686889
Kahama,Shinyanga , Tanzania

Post a Comment

HOME

 
Top