0

VYUNGU VYA RUNGEMBA NI ZAIDI YA UTALII WILAYA YA MUFINDI

Mmiliki  wa mtandao wa matukiodaima akiwa ameshika kiatu cha michezo (njumu) ya asili  kilichotengenezwa kwa  udongo  ambacho  kinauzwa kati ya Tsh  150,000 kwa  kimoja na  pea moja ni Tsh 300,000.kiatu  hiki ni  moja kati ya  vivutio vya utalii katika  wilaya ya Mufindi  mkoani Iringa vinavyotengenezwa  eneo la Rungemba na kuvutia  watalii  wa ndani na nje.
Baadhi ya  vifaa mbali mbali  vilivyotengenezwa kwa udongo  eneo la  Rungemba  Mufindi  ni  zaidi ya  utalii 
Majiko  na  vyungu vilivyotengenezwa kwa  udongo.
Mmoja kati ya  wanahabari  mkoani Iringa  Mawazo Marembeka akitazama  vyungu eneo la  Rungemba Mufindi mkoani Iringa.
Afisa utalii kanda  ya  kusini Tanapa  Bi Risala Kabongo (kushoto)  akitazama  vyungu na  dhana  mbali mbali za  kitalii  eneo la  Rungemba.
Kiatu  kilichotengenezwa  kitalii  zaidi kwa udongo.

Na  MatukiodaimaBlog
VYUNGU vya  asili   vinavyotengenezwa  kijiji  cha Rungemba katika  wilaya ya  Mufindi  mkoani  Iringa  vinaweza  kusaidia  kuitangaza  wilaya ya  Mufindi kiutalii  zaidi  iwapo  serikali  ya  wilaya  hiyo  itawawezesha  na  kuwahamasisha  zaidi  wananchi  wilayani  humo  kujiajili wenyewe katika ufinyanzi.

Kijiji  hicho  cha Rungemba ambacho kwa sasa  wananchi  wake hasa wanawake  wameendelea  kujipatia  kipato  zaidi kutokana na ufinyanzi  wa  vyungu na mapambo  mbali mbali  yatokanayo na ufinyanzi ,kimeendelea  kujipatia wageni  zaidi  wa ndani na nje  ambao  wamekuwa  wakifika  kupata  huduma  ya  kazi itokanayo na ufinyanzi.

Akizungumza na mtandao  www.matukiodaima.co.tz mmoja  kati ya  wanawake  wanaojishughulisha na  ufinyanzi  wa  vyungu eneo hilo Bi Anna Kalinga alisema kuwa awali  walianzisha  eneo  hilo kama  utani  utani  ila  kwa  sasa  eneo  hilo  limeendelea  kupata  umaarufu mkubwa na hata  gharama za  vyungu na  mapambo  mengine  imeendelea kukua zaidi.

Hata   hivyo  alisema  kuwa  idadi ya  wananchi  kupenda  kutengeneza vitu  vya utalii  kwa  kutumia udongo  imeendelea  kuongezeka huku baadhi ya  watu  wameanza  kuboresha maisha  yao kwa  kujenga  nyumba za kisasa na kusomesha  watoto  kupitia kazi za ubunifu  wa kitalii.

Alisema katika   eneo hilo  wanatengeneza  vitu  mbali mbali za kitalii  vikiwemo  vitu mfano  wa viatu vya  kupandia maua  ambavyo  gharama  yake ni kati ya 160,000 hadi  320,000  kwa viatu  viwili  kwa maana ya pea  moja huku  vyungu  vimekuwa  vikiuzwa kati ya  shilingi  45,000 hadi 75,000 na kuwa  bei  hiyo  imepandishwa kutokana na ongezeko  la  watalii katika  eneo hilo .

" Eneo   hili kwa  sasa limeendelea  kuwa maarufu  sana  kwa kutangaza  utalii   na utamaduni  wa kitanzania  kupitia ufinyanzi  ila  bado serikali haijatambua na  kuelekeza  nguvu  zake  zaidi  eneo  hilo kwa kuweka  utaratibu mzuri  wa kuvutia watalii  kufika  hapa"

Mkuu  wa  wilaya ya  Mufindi  Evarista  Kalalu  akizungumzia  utalii  wa eneo hilo alisema  wilaya  yake  ilianza mchakato  wa  kubainisha  vivutio  vya utalii pamoja na  kukusudia  kushirikiana na familia ya Chifu Mwinyigumba  ili  kuweka mazingira mazuri eneo la  makaburi kama  sehemu ya historia  pindi  watalii  wanapofika  kutembelea   eneo  hilo.

Wakati kwa upande wa   wasanii  hao  wanaotangaza  wilaya  kupitia  ufinyanzi  za  vitu mbali mbali za  utalii alisema ofisi yake  ilianza mwaka 2007  kwa  kuwapeleka   baadhi ya  wana kikundi  Kyela  mkoani Mbeya  kujifunza namna ya  utengenezaji  wa  vyungu  bora  na dhana  nyingine ili  kuvutia  watali zaidi  japo kwa  sasa  wilaya  hiyo haina  afisa utalii baada ya  aliyekuwepo  kufariki  dunia mwaka jana .


Afisa utalii kanda  ya  kusini Tanapa  Bi Risala Kabongo alisema  kuwa   eneo hilo la Rungemba ni moja kati ya maeneo ya  vivutio vya  utalii katika mikoa ya  kusini na kuwa  wilaya ya  Mufindi  pamoja na  vivutio vingine  bado  wanapaswa  kuboresha  eneo  hilo ili  kulitumia kama  sehemu ya utalii  na kuwa suala la  utalii  linajumhisha mambo mbali mbali yakiwemo ya hoteli ,biashara  na wanyama  ,maji ,tamaduni ,na mambo mengine  mengi ambayo wageni  hupenda  kujifunza .

Post a Comment

HOME

 
Top