RAIS KIKWETE AWASILISHA RIPOTI YA KAMATI YA VIONGOZI JUU YA MABADILIKO YA TABIA NCHI KATIKA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA UMOJA WA AFRIKA ULIOFANYIKA ADDIS ABABA ETHIOPIA
Mwenyekiti wa Kamati ya Viongozi wa Afrika Juu ya mabadiliko ya Tabia nchi Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasilisha ripoti ya utendaji wa kamati hiyo katika Mkutano wa Viongozi wa Umoja wa Afrika uliofanyika jijini Addis Ababa Ethiopia.Mkutano huo ulimalizika January 31,2015
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 24 wa kawaida wa wakuu wa nchi wanachama wa umoja wa Afrika unaofanyika katika mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa
Mwenyekiti wa Kamati ya Viongozi wa Afrika Juu ya mabadiliko ya Tabia nchi(The Committee of African Heads of State and governments on Climate change) Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimakabidhi nakala ya Ripoti ya utendaji mwenyekiti mpya wa kamati hiyo Rais wa Misri Abdel Fattah el Sisi wakati wa Mkutano wa wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika uliofanyika Addis Ababa Ethiopia.Rais Kikwete alipongezwa kwa kuiwezesha kamati hiyo kupata mafanikio makubwa.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na mwenyeji wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn muda mfupi kabla ya kumalizika kwa mkutano wa 23 wa kawaida wa wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika ulifanyika katika mji Mkuu wa Ethiopia Addis Ababa,
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Malawi Profesa Peter Mutharika (kulia) wakikutana na marais wastaafu, Thabo Mbeki wa Afrika ya Kusini (Kushoto) na Joachim Chissano wa Msumbiji (wapili kushoto) wakati wa mkutano wa 24 wa kawaida wa wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika unaofanyika Addis Ababa Ethiopia
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais wa Malawi Professa Peter Mutharika (Wanne kushoto), Rais mstaafu wa Msumbiji Joachim Chissano, Rais mstaafu wa Afrika ya Kusini Thabo Mbeki (kulia) pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya kukutana wakati wa mkutano wa wakuu wan chi wanachama wa AU unaofanyika jijini Addis Ababa Ethiopia (PICHA NA IKULU)
Post a Comment
HOME