AIRTEL YATOA VITABU VYA SAYANSI SEKONDARI BARIADI SIMIYU
Mkuu
wa wilaya ya Bariadi Bw. Erasto Sima akisoma Hotuba katika makabidhiano
ya msaada wa vitabu vya masomo ya sayansi kwa shule ya sekondari Bariadi
uliotolewa na kampuni ya Airtel Tanzania.
Mkuu
wa shule ya sekondari ya Bariadi Bw. Pawa Lutema akipokea msaada wa
vitabu vya sayansi kutoka kwa mkuu wa wilaya Bariadi, Vitabu hivyo vyote
vinathamani ya sh milioni 6 na ni vya masomo ya sayansi kutoka kampuni
ya simu ya Airtel kupitia mradi wake wa kusaidia elimu wa Airtel Shule
yetu.
Meneja
wa Airtel Simiyu Bw. Ezekiel Nungwi akikabidhi msaada wa vitabu vya
sayansi vyenye thamani ya milioni 6 kwa Mkuu wa wilaya ya Bariadi Bw.
Erasto Sima, vitabu hivyo ni sehemu ya msaada wa Airtel kupitia mradi
wake wa Airtel shule yetu.
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel imepiga jeki jitihada za serikali za
kuhamasisha masomo ya sayansi kwa kutoa msaada wa vitabu vya sayansi kwa
shule ya sekondari ya Bariadi iliyopo Mkoani Simiyu.
Msaada
huo wenye thamani ya shilingi milioni 6 unahusisha vitabu vya fizikia,
hisabati, baiolojia na kemia kwa ajili ya wanafunzi wanaosoma masomo
hayo shuleni hapo.
Akipokea
msaada huo mkuu wa wilaya ya Bariadi Bw. Erasto Sima amesema shule
nyingi wilayani humo zimekuwa zikikabiliwa na changamoto ya upungufu wa
vitabu vya masomo ya sayansi licha ya kwamba kuna uhaba pia wa walimu wa
masomo hayo.
“Ni
kweli kwamba uhaba wa vitabu unakwamisha kwa kiasi kikubwa wanafunzi
kujifunza kwa ufasaha masomo ya Sayansi wilayani Bariadi hali
inayorudisha nyuma ukuaji wa elimu ya sayansi wilayani hapa”. Alisema
Bwana Sima.
“uhaba
wa vitabu ni moja ya changamoto, lakini uhaba wa walimu wa masomo ya
sayansi ni kikwazo kikubwa kwa utoaji wa elimu ya sayansi kwa wanafunzi
wetu hapa Bariadi” aliongeza Bwana Sima.
Aidha
Bw. Sima ameishukuru kampuni ya simu ya airtel kwa kuona umuhimu wa
kuboresha masomo ya sayansi ambayo ufaulu wake umekuwa mdogo hali
ambayo inayotoa fursa kwa wanafunzi kujifunza kwa umakini zaidi.
“Msaada
huu utaongeza hamasa kwa wanafunzi wetu kujifunza masomo ya sayansi
hivyo tunawashukuru sana Airtel kwa kuona umuhimu wa kusaidia shule hii
na hasa vitabu vya sayansi” alimalizia Bwana Sima.
Kwa
upande wake mkuu wa shule ya sekondari Bariadi Bw. Pawa Lutema akipokea
vitabu hivyo, amesema hatua hiyo ni sehemu ya utatuzi wa changamoto ya
vitabu vya sayansi na kisha kuahidi kuvitunza ili viwe msaada kwa
wanafunzi watakaosoma shuleni hapo.
Awali
meneja wa Airtel Mkoani Simiyu Bw. Ezekiel Nungwi akikabidhi msaada
huo wa vitabu amesema kuwa kampuni yake inaendelea tena katika mwaka
huu wa 2015 na mpango wake wa kutoa msaada wa vitabu kwenye shule
mbalimbali nchini kwa lengo la kusaidia ukuaji wa elimu nchini.
Msaada
huo wa vitabu vya masomo ya hisabati,kemia,fizikia na Bailojia
utasaidia kupunguza uhaba wa vitabu vya sayansi kwenye shule hiyo.
Airtel
pia kupitia mfuko wake huo wa Airtel Shule yetu mwezi huu imejipanga
kukabidhi vitabu katika mikoa mingine miwili ikiwemo Kilimanjaro na
Arusha ambapo inatarajiwa kuzifikia zaidi ya shule zingine sita.
Post a Comment
HOME