KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA AENDELEA NA ZIARA YAKE MKOA WA KASKAZINI UNGUJA LEO
Baadhi
ya Vijana wa CCM wakishangilia ujio wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana
na ujumbe wake.alipowasili Kikobweni katika ukumbi wa MKorea,Wilaya ya
Kaskazini A,mkoa wa Kaskazini Unguja.
Ktibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa ameambatana na Wanachama wa kikundi
cha Ushirika wa Tuko Imara mara baada ya kushiriki kupanda
Migomba,katika Kijiji cha Banda Maji,Wilaya ya Kaskazini A mkoa wa
Kaskazini Unguja mapema leo.
katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki kupanda Mgomba katika shamba la
Kikundi cha Ushirika wa Tuko Imara unaojishughulisha na Kilimo cha
Migomba na Mbogamboga katika Kijiji cha Banda Maji,Wilaya ya Kaskazini A
mkoa wa Kaskazini Unguja mapema leo.
Mbunge
wa Jimbo la Chaani,Mh.Ally Juma Haji a.k.a Chepe akizungumza na baadhi
ya vijana kuhusiana mambo mbalimbali ikiwemo na kuwahimiza kupiga kura
ya ndio kwa katiba inayopendekezwa.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki ujenzi wa tawi la CCM Chaani
Masingini,jimbo la Chaani ambapo pia alipokea taarifa ya ujenzi wa tawi
hilo na kusalimiana na Wananchi,Wilaya ya Kaskazini A,mkoa wa Kaskazini
Unguja.
Msafara wa Katibu Mkuu,Ndugu Kinana ukielekea kwenye Mradi huo wa ujenzi wa barabara unaofadhiriwa na TASAF
Baadhi
ya Wananchi wanaoshiriki kazi ya ujenzi wa barabara katika kijiji cha
Kijini kwa Shauripili,jimbo la Shaani,wilaya ya Kaskazini A,mkoa wa
Kaskazini Unguja inayojengwa kwa mradi wa TASAF,wakimsikiliza Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipozungumza nao mapema leo.Barabara hiyo
yenye urefu wa kilometa 1.7 ina thamani ya shilingi milioni 26
Katibu
mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki kazi ya ujenzi wa barabara katika
kijiji cha Kijini kwa Shauripili,jimbo la Shaani,wilaya ya Kaskazini
A,mkoa wa Kaskazini Unguja inayojengwa kwa mradi wa TASAF,barabara hiyo
yenye urefu wa kilometa 1.7 yenye thamani ya shilingi milioni 26
Mradi
wa ujenzi wa Nyumba ya Madaktari inayojengwa katika Sheia ya Kijini
katika jimbo la Matemwe,Wilaya ya Kaskazini A,mkoa wa Kaskazini
Unguja,yenye thamani ya shilingi milioni 80 ukiendelea,Mradi huo
umejengwa kwa nguvu za Wananchi na Serikali pia.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki ujenzi wa Nyumba ya
Madaktari inayojengwa katika Sheia ya Kijini,jimbo la Matemwe,Wilaya ya
Kaskazini A,mkoa wa Kaskazini Unguja,yenye thamani ya shilingi milioni
80.Mradi huo huo umejengwa kwa nguvu za Wananchi na Serikali pia.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na viongozi wengine wa CCM,wakitazama mchezo
wa sarakasi unaofanywa na vijana mara baada ya kupokea taarifa fupi ya
ujenzi wa wa jengo la ya Nyumba ya Madaktari inayojengwa katika Sheia
ya Kijini katika jimbo la Matemwe,Wilaya ya Kaskazini A,mkoa wa
Kaskazini Unguja,yenye thamani ya shilingi milioni 80,nyumba mradi huo
umejengwa kwa nguvu za Wananchi na Serikali pia.
Baadhi
ya viongozi wa timu za mpira wakiwa na vifaa mbalimbali walivyopokea
kutoka kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana,mara baada ya kukagua na
kushiriki kazi ya ujenzi wa uzio wa Uwanja katika sheia ya Tazari,jimbo
la Nungwi mkoa wa Kaskazini Unguja
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Wananchi wa Kigunda,mara baada
ya kupokea taarifa fupi ya jengo la SACCOS ya vijana yenye Wanachama
114.SACCOS hiyo imeanzishwa kwa ajili ya kuisaidia jamii katika suala
zima la kuweka unafuu wa kukopa kirahisi.
Balozi
wa Shina namba 3,Balozi Khamis Makame Faki akizungumza mbele ya Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na baadhi ya wananchi na wanachama,katika jimbo
la Nungwi,wilaya ya Kaskazini A,Mkoa wa Kaskazini Unguja,Ndugu Kinana
alifika kwa balozi huyo na kukagua uhai wa chama na Wanachama.
katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Banda
Maji mara baada ya kupokea taarifa ya kikundi cha ushirika wa Tuko Imara
unaojishughulisha na Kilimo cha Migomba na Mbogamboga,pia kushiriki
kazi ya kilimo cha Migomba na Mbogamboga,katika Wilaya ya Kaskazini A
mkoa wa Kaskazini Unguja mapema leo.
Post a Comment
HOME