MKUTANO WA BARAZA LA PILI LA WAFANYAKAZI WA OFISI YA TAIFA YA UKAGUZI WAFUNGULIWA RASMI
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais, Utawala Bora Mhe. George Mkuchika, (katikati)
akiwa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Mussa Juma Assad
(kushoto) pamoja na wajumbe wengine wakiimba wimbo wa wafanyakazi wakati
wa Mkutano wa Pili wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya
Ukaguzi uliofanyika jana katika Ukumbi wa Hoteli ya Naf Beach iliyoko
mkoani Mtwara.
Mkaguzi
na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Mussa Juma Assad akisoma
hotuba ya kumkaribisha mgeni rasmi wakati wa Mkutano wa Pili wa Baraza
la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi uliofanyika jana katika
Ukumbi wa Hoteli ya Naf Beach iliyoko mkoani Mtwara.
Mgeni
rasmi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utawala Bora Mhe. George Mkuchika,
akiwahutubia wajumbe wa Baraza la Pili la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa
ya Ukaguzi muda mchache kabla ya kulifungua baraza hilo jana katika
Ukumbi wa Hoteli ya Naf Beach iliyoko mkoani Mtwara.
Wajumbe
wa Baraza la Pili la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi
wakimsikiliza kwa makini Mgeni rasmi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,
Utawala Bora Mhe. George Mkuchika (hayupo pichani) wakati wa mkutano wa
baraza hilo uliofanyika jana katika Ukumbi wa Hoteli ya Naf Beach
iliyoko mkoani Mtwara. (PICHA ZOTE NA SARAH REUBEN - OFISI YA TAIFA YA
UKAGUZI).
Na: Evelyn Thomas - Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi - Mtwara.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais, Utawala Bora Mhe. George Mkuchika (Mb) amefungua
mkutano wa Baraza la Pili la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi
uliofanyika jana mkoani Mtwara.
Katika
mkutano huo, Waziri Mkuchika ameipongeza ofisi hiyo kwa kufanya ukaguzi
wenye viwango vya juu na hatimaye kupungua kwa hati chafu au zenye
mashaka katika Serikali Kuu na Serikali za Mitaa.
"Mimi
binafsi najivunia sana kutokana na jitihada na mafanikio ya kazi za
Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi ambayo yameijengea heshima nchi yetu na
ulimwengu kwa ujumla, licha ya kupungua kwa hati chafu, hivi sasa Nchi
yetu, ikiwakilishwa na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, inakagua shughuli za
Umoja wa Mataifa jambo ambalo ni la kujivunia sana", amesema Waziri
Mkuchika.
Mkuchika
ameongeza kuwa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi ni chombo nyeti sana, si hapa
Tanzania tu bali katika nchi zote zinazozingatia demokrasia,uwajibikaji
na uwazi, katika mapato na matumizi ya rasilimali za umma ili kuleta
maendeleo ya watu wake.
Akizungumza
wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi, Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
Prof. Mussa Juma Assad amesema mkutano huo una dhumuni la kutoa fursa
kwa watumishi, kupitia wawakilishi wao, kujadiliana juu ya masuala
mbalimbali ya msingi yanayohusu tija na ufanisi mahali pa kazi.
"
Dhana ya kuwa na Mabaraza ya Wafanyakazi katika sehemu za kazi, hasa
katika utumishi wa umma ina lengo la kutoa fursa kwa watumishi, kupitia
wawakilishi wao, kujadiliana juu ya masuala mbalimbali ya msingi
yanayohusu tija na ufanisi kwa upande mmoja na upande mwingine maslahi
yao kama watumishi", amesema Prof. Assad.
Prof.
Assad amefafanua kuwa mkutano huu wa Baraza la Wafanyakazi utatumika
kujadili malengo na mipango ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi ikiwa ni pamoja
na Maslahi ya Watumishi kwa ujumla.
Mkutano
wa Baraza la Pili la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi
utamalizika leo jioni ambapo kaulimbiu ya mwaka huu ni “Weledi na
nidhamu katika kutekeleza majukumu ya Utumishi wa Umma ni chachu ya
kutoa huduma bora kwa wananchi.”
Post a Comment
HOME