Saccoss za Vijana katika Halmashauri ni muhimu kwa vijana
Kijana
Andrew Mlaki kutoka kikundi cha Akili ni Mwanga akielezea vijana
wenzake (hawapo pichani) shughuli zinazofanywa na kikundi chake baada ya
kikundi hicho kutembelewa na wawezeshaji waliofika Wilaya ya Mwanga
kuhamasisha vijana na kuwapa elimu kuhusu ujuzi na stadi za maisha.
Kushoto ni mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Bibi. Ester Riwa.
Afisa
Vijana wa Wilaya ya Mwanga Bibi Subira Mfanga akizungumza na vijana
walioshiriki semina ya uhamasishaji kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana
Mkoani Kilimanjaro katika Wilaya ya Mwanga.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Bw. Jamhuri David Willium (katikati)
akisikiliza mrejesho kutoka kwa wawezeshaji wa Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo waliofika ofisini kwake baada ya kufunga
semina ya uhamasishaji kwa Vijana wa Wilaya za Mwanga na Moshi Vijijini
hivi karibuni.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Bw. Jamhuri David Willium kushoto
akipokea Sera ya Maendeleo ya Vijana kutoka kwa mwezeshaji wa Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa baada ya kufunga
semina ya uhamasishaji kwa Vijana wa Wilaya za Mwanga na Moshi Vijijini
hivi karibuni.
Wawezeshaji
kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Maafisa Ushirika
na Maafisa Vijana kutoka Wilaya ya Mwanga na Moshi Vijijini, katika
picha ya pamoja na baadhi ya Vijana wa Wilaya hizo walioudhuria semina
ya uhamasishaji kwa vijana kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana katika
Wilaya ya Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro. (Picha zote na : Genofeva Matemu – Maelezo)
Vijana wa Mkoa wa Kilimanjaro wameziomba Halmashauri zao kuhamasisha vijana kuanzisha Saccoss za Wilaya zitakazowawezesha vijana kuwekeza na kuwasaidia kuomba mkopo wa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana utakaopitishiwa katika Saccoss hizo ili waweze kujiajiri wenyewe na kuondokana na umasikini.
Hayo yamesemwa na Vijana wakati wa kufunga semina ya uhamasishaji kwa vijana kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana na kuiomba Wizara yenye dhamana na vijana kujitolea kutoa elimu kwa vijana mara kwa mara itakayowawezesha vijana kujitambaua na kuwajengea uwezo.
Akizungumza baada ya kufunga semina hiyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Bw. Jamhuri David Willium ameishukuru timu kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuweza kufika katika Halmashauri yake na kuwaomba kujitolea pale Wilaya itakapowahitaji kwa mara nyingine kwa ajili ya kuelimisha vijana wa Mwanga.
Bw. Willium amesema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga ipo karibu na vijana wake, imeweza kuwaunganisha vijana kwenye vikundi mbalimbali na kuwashirikisha vijana katika shughuli mbalimbali za maendeleo zinazofanywa na Halmashauri hiyo hivyo kuwahaidi vijana kushughulikia ufunguaji ya Saccoss ya vijana kwa maendeleo ya vijana wa Mwanga.
“Vijana ni taifa la leo, sisi kama viongozi wa Halmashauri tupo tayari kushirikiana nao kwa jitihada zote kwani umuhimu wa Saccoss ya vijana katika Halmashauri tunaufahamu hivyo tutajitahidi kusimamia suala la ufunguzi wa Saccoss ya vijana itakayowawezesha kujitegemea kwa maendeleo yao na maendeleo ya Wilaya ya Mwanga”, amesema Bw. Willium.
Naye mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Ester Riwa ameuomba uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga kushirikiana na wadau wengine wanaojishughulisha na masuala ya vijana kuwasaidia Vijana wa Mwanga huku wakitumia vyombo vya habari kuelimisha vijana na kubadili fikra za vijana kuwa chanya.

Post a Comment
HOME