CHANGAMOTO ZA WATANZANIA KATIKA MAONESHO YA KIMATAIFA YANAYOFANYIKA MASCUT - OMAN
Wageni
mbalimbali wakiingia na kutoka Katika Banda la Watanzania kujione
bidhaa za Watanzania Wanaoshiriki katika Maonesho ya Kimataifa ya
Sanaa,Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea Mascut-Oman.
Msanii
wa kuchora Fred Halla akifanya sanaa yake ya Uchoraji katika Katika
Banda la Watanzania.Fred ni mmoja wa Watanzania Wanaoshiriki katika
Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa,Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea
Mascut-Oman.
Msanii
wa Uchongaji Iddy Amana akiwahudumia wateja katika Banda la Watanzania.
Iddy ni mmoja wa Watanzania Wanaoshiriki katika Maonesho ya Kimataifa
ya Sanaa,Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea Mascut-Oman.
Mpishi
wa Vyakula mbali mbali Haji Omar akiwahudumia wateja wake wanaopenda
vyakula vya Kitanzania.Haji ni mmoja wa Watanzania Wanaoshiriki katika
Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa,Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea
Mascut-Oman.
Baadhi
ya Wateja wa Vyakula vya kitanzania wakila chakula chenye Asili ya
Tanzania,Zanzibar (Urojo) katika Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa,Ubunifu
na Utamaduni yanayoendelea Mascut-Oman.
Mkuu
wa Msafara wa Watanzania Wanaoshiriki katika Maonesho ya Kimataifa ya
Sanaa,Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea Mascut-Oman Bi Khadija Bhatashy
akiulizia bei ya bidhaa katika Banda la Iran. Iran ni moja ya nchi
washiriki wa Maonesho hayo. Picha na Faki Mjaka-Mascut Oman.
Na Faki Mjaka-Mascut Oman
Kukosekana
kwa Semina ya pamoja na uelewa mdogo wa lugha ya Kiarabu ni miongoni
mwa Changamoto zinazowakabili Wajasiriamali wa Kitanzania wanaoshiriki
Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa na Utamaduni nchini Omani.
Hayo
yameelezwa na Watanzania wanaoshiriki Maonesho hayo yanayoendelea kwa
muda wa mwezi mmoja na kushirikisha Mataifa mbalimbali.
Mmoja ya Wajasiriamali hao Kulthum Mohamed amesema uelewa mdogo wa lugha
ya Kiarabu ni changamoto kwake inayomkabili katika kutoa ufafanuzi wa
baadhi ya Bidhaa alizokuwa nazo.
Mjasiri
Amali huyo wa Viungo (spices) amedai kuwa licha ya baadhi ya Waarabu
kujua Lugha ya Kiswahili amebaini hawapendi kuzungumza jambo ambalo
linawapa shida.
“Licha ya hawa WaomanI kukijua Kiswahili lakini wengi wao wanavyofika
hapa wanajifanya hawakijui jambo ambalo linatukwaza kidogo katika kutoa
ufafanuzi wa Bidhaa zetu kwa Lugha ya Kiarabu” Alisema Kulthum.
Aidha K
amebaini kuwa hakukuwa na Semina ya Pamoja ya Washiriki kujua mambo
mbalimbali na Vipaumbele vya Waarabu jambo ambalo lingeweza kuwajengea
uelewa mpana wa Waoman nakujua Bidhaa muhimu zaidi za kuja nazo katika
Maonesho hayo.
Kwa upande wake Mkuu wa Msafara huo wa Watazania katika Maonesho hayo ya
Utamaduni na Sanaa Bi Khadija Battashy amesema kuna baadhi ya Bidhaa
ambazo haziendani sana na Utamaduni wa Omani kama vile nguo za kike
zenye Mikono Mifupi.
“Kwa
mfano utakuta baadhi ya Nguo tulizokuja za kike nyingi zao
zimetengenezwa zikiwa na Mikono mifupi tena zimepasuliwa sasa kwa
Utamaduni wao hawa hawazipendelei sana,nadhani tungetengeneza za Mikono
mifupi Wangezipenda zaidi” Alisema Bi Khadija Battashy.
Hata
hivyo anaamini Tanzania itafanya vyema katika Monesho hayo na hata
kuibuka Mshindi wa mwanzo ikiwa kutatokea kutangazwa mshindi.
Kwa upande wake Mjasiriamali wa Bidhaa za Nguo Bi Anna Matinde amesema
ana matumaini makubwa kuwa Bidhaa za Tanzania zitapata Wateja kutoka na
ubora wake.
“Mi
naamini Bidhaa zetu ni bora na zitapata Wateja maana hata hiyo Mishahara
ya Waarabu bado tunaamini ikitoka watazidi kununua bidhaa zetu”
Aliongeza Bi Anna.
Kwa Upande wao Wageni wanaolitembelea Banda la Tanzania wamelisifia
kutokana na kuwa na bidhaa bora na za upekee zikiwemo za Viungo kama
vile Karafuu na Mavazi ya Kimasai.
Maonesho
hayo ya Muda wamwezi mmoja ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika
katika Jimbo la Al-Amerat mjini Mascut, huanza kila ifikapo saa 10
jioni na kufungwa saa nne usiku kwa Majira ya Oman ambapo Nchi
mbalimbali Washiriki huonesha Bidhaa zilizotengenezwa kwa Mikono
zinazowakilisha Utamaduni wao na Watu hununua Bidhaa hizo.
Post a Comment
HOME