BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA AFANYA ZIARA MKOANI KAGERA KUKAGUA ENEO LA KUJENGA CHUO CHA KISASA CHA UFUNDI (VETA) NA KUONA FURSA ZA UWEKEZAJI KATIKA MKOA
Balozi
wa China nchini Tanzania,LU Youqing akicheza ngoma ya asili ya Mkoa wa
Kagera wakati alipokuwa akilakiwa kwenye uwanja wa ndege wa
Bukoba.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, John Mongella .
Mkuu
wa Mkoa wa Kagera, John Mongella akimkabidhi Balozi wa China nchini
Tanzania,LU Youqing Hati na ramani eneo lililotengwa na serikali ya mkoa
kwa ajili ya kujenga chuo cha Ufundi (VETA) cha Kitaifa kilichoahidiwa
na serikali ya China wakati wa ziara ya Rais Kikwete nchini humo mwaka
jana.
Balozi
wa China nchini Tanzania,LU Youqing akipokea zawadi ya ramani ya Afrika
Mashari iliyochorwa kutoka kwa wanafunzi wa shule ya Mgeza Mseto.
Balozi LU akisaini kitabu cha wageni Bukoba airport.
Balozi wa China nchini Tanzania,LU Youqing akitoa zawadi kwa wanafunzi.
Picha ya Pamoja.
Balozi
wa China nchini Tanzania,LU Youqing yupo mkoani Kagera kwa ziara ya
siku mbili kukagua eneo lililotengwa na serikali ya mkoa kwa ajili ya
kujenga chuo cha Ufundi (VETA) cha Kitaifa kilichohaidiwa na serikali ya
China wakati wa ziara ya Rais Kikwete nchini humo mwaka jana Oktoba
2014.
Akimkaribisha
mkoani Kagera Mkuu wa Mkoa John Mongella alimweleza Balozi LU kuwa mkoa
wa Kagera una fursa nyingi za uwekezaji ambazo ni pamoja na uwekezaji
katika viwanda vidogo vidogo vya kusindika bidhaa mbalimbali ili kuinua
uchumi wa wananchi na mkoa kwa ujumla.
Bw.
Mongella alimwomba Balozi LU kufikiria kuleta wataalamu wa afya hasa
madaktari kutoka nchini mwake hususani katika hospitali ya Rufaa ya mkoa
ili kutoa huduma kwani mkoa upo mbali sana na hospitali za Rufaa za
taifa jambo ambalo huleta usumbufu kwa wagojwa wanaohitaji huduma za
hospitali za rufaa.
Balozi
LU katika kutoa salaamu zake alisema kuwa amefurahi kufika mkoani
Kagera kwa mara ya pili na akasifu mkoa kwa kuwa na hali nzuri ya hewa
na kubarikiwa katika nyanja mbalimbali za kiuchumi. Aidha, alisema
kutokana na urafiki wa nchi mbili za Tanzania na China amefurahi kuwa
sasa kutakuwa na alama ya urafiki huo katika mkoa wa Kagera.
Pamoja
na kuusifia Mkoa wa Kagera imeisifia serikali ya Tanzania kwa
kutekeleza miradi ya maendeleo,alisema kuwa ukipita mikoani unaona
mabadiliko makubwa kuliko ilivyokuwa hapo nyuma. Ambapo alisema kuwa
serikali ya China imewekeza na kutekeleza miradi ya maendeleo nchini
Tanzania yenye thamani ya bilioni 3.15 dolla za kimarekani kwa mwaka
2013/2014.
Balozi
LU alitembelea kiwanja cha hekta 26,000 kilichopo eneo la Kahororo
katika Halamashauri ya Manispaa ya Bukoba ambapo chuo cha ufundi (VETA)
kitajengwa na kujionea mwenyewe kitakapojengwa chuo hicho. Pia
alitembelea shule ya Mgeza Mseto ambako aliwahi kutembelea na kutoa
msaada wa komputa ili kuona wanafunzi wa shule hiyo maendeleo yao.
Katika
shule ya msingi Mgeza Mseto yenye wanafunzi wa bweni na kutwa pia
inapokea watoto wa aina tatu, watoto wenye albinisimu, watoto wenye
ulemavu wa viungo, na watoto wa kawaida, Balozi LU alisema amefurahi
kuwaona tena na kuhaidi kutoa msaada zaidi wa komputa ili watoto waweze
kila mmoja kujifunza komputa.
Katika
maelezo yake Balozi LU aliufananisha mkoa wa Kagera na Jimbo la Chandog
la nchini China na kusema kuwa atahakikisha unaungaisha urafiki kati ya
mkoa wa Kagera na jimbo hilo ili kuleta maendeleo zaidi Kagera.
Vilevile alisema atahakikisha anfanya mpango wa Tanzania hasa mkoa wa
Kagera unakuwa na utaratibu wa kubadilishana walimu kutoka nchini China.
Maeneo
ya uwekezaji ambayo mkoa umeyatenga kwa ajili ya uwekezaji ni pamoja na
Kilimo cha kisasa katika maeneo mbalimbali, Ufugaji wa kisasa wa
samaki, Ujenzi wa bandari ya Kemondo(contena terminal) na ufugaji wa
kisasa wa nyuki pamoja na ujenzi wa chuo cha ufundi (VETA)
Post a Comment
HOME