0

Ishu ya kukamatwa Prof. Lipumba jana imefika Bungeni na kuibua mvutano mwingine!

.
Prof. Lipumba akiwa ndani ya gari ya Polisi baada ya kukamatwa jana.
Jana January 27 kulikuwa na taarifa kuwa Jeshi la Polisi lilitumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa Chama cha CUF waliokuwa wanaenda kushiriki katika mkutano wa kuwakumbuka wanachama wenzao waliouwawa Zanzibar mwaka 2001, pamoja na kuwatawanya Waandishi wa Habari huku Mwenyekiti wa Chama hicho Prof. Ibrahim Lipumba na viongozi wengine kuwekwa chini ya ulinzi wa Polisi.
Ishu hiyo leo imefika katika kikao cha Bunge, Jana tar 27 January mwaka huu Wilayani Temeke Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chama cha CUF Prof. Ibrahim Lipumba alikuwa na ratiba ya kufanya mkutano wa hadhara pamoja na maandamano… walifuata taratibu zote za kisheria na za kikatiba… La kushangaza dakika za mwisho Jeshi la Polisi walikataza jambo hilo lisiendelee na Prof. Lipumba akaonyesha ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwa kutokuendelea na jambo hilo, lakini Jeshi la Polisi likafika baadae kidogo wakaamua kutumia nguvu dhidi ya raia ambao hawafanyi fujo yoyote, raia ambao walionyesha ushirikiano na utii kwa Jeshi la Polisi, wakaamua kumpiga Prof. Lipumba, wakawapiga wanachama na raia  wengine wa Tanzania hata watoto wadogo chini ya umri wa miaka 5 wakapigwa mabomu, Waandishi wa Habari wakapigwa virungu kwa kudhalilishwa sana.. jambo hili linaondoa Utulivu, Amani na kuaminiana kwa Taifa letu“– Mbunge James Mbatia.
Kuwa Jeshi la Polisi lilisema lenyewe jana kwamba ni agizo kutoka juu, tunataka tujue hilo agizo kutoka juu ni kwa nani, kwa sababu gani na kwa maslahi gani? Naomba Mheshimiwa Spika kutoa hoja  tuahirishe shughuli za Bunge tulijadili jambo hili kwa maslahi mapana kwa Taifa letu, tulijadili jambo hili ili tuweze kupata majibu sahihi na tuhakikishe kwamba jambo hili halitajitokeza” — James Mbatia
Mbunge James Mbatia
Mbunge James Mbatia
Akijibu kuhusu ishu hiyo Spika Makinda akasema;Ninachosema jambo hili ni kubwa sana, hatuwezi kuzungumza kama mnavyozungumza saa hizi, ni vizuri watu wote wakaelewa tutazungumza na mtoa hoja Mbatia tumezungumza akiwepo Tundu Lissu, Engineer Mnyaa na ndio mimi nimewaruhusu kwamba hili suala Mbatia atasema halafu naitaka Serikali nimesema kesho na kesho tutatenga wakati
Spika Anne Makinda
Spika Anne Makinda.
Wabunge walionekana kupingana na majibu ya Spika Makinda, ikatangazwa kuahirishwa kikao hicho; “Naahirisha  bunge mpaka saa kumi“–  Spika Anne Makinda.

Post a Comment

HOME

 
Top