Kupunguza umasikini kuendelea kuwa lengo kuu la milenia- UN
Ofisa Habari Umoja wa Mataifa (UN), Bi. Usia Nkhoma Ledama akizungumza
na washiriki wa Uzinduzi wa Kampeni ya Chukua Hatua Dhidi ya Umasikini
2015, iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wananchi waslioshiriki katika Uzinduzi wa Kampeni ya Chukua
Hatua Dhidi ya Umasikini 2015, iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali walioshirii atika Uzinduzi wa
Kampeni ya Chukua Hatua Dhidi ya Umasikini 2015, iliyofanyika jijini Dar
es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali wakiwakatika maumbo ya kuunda
neno '2015' kuashiria uzinduzi wa Kampeni ya Chukua Hatua Dhidi ya
Umasikini 2015, iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali wakiwakatika maumbo ya kuunda
neno '2015' kuashiria uzinduzi wa Kampeni ya Chukua Hatua Dhidi ya
Umasikini 2015, iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali wakiwakatika maumbo ya kuunda
neno '2015' kuashiria uzinduzi wa Kampeni ya Chukua Hatua Dhidi ya
Umasikini 2015, iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali wakiwakatika maumbo ya kuunda
neno '2015' kuashiria uzinduzi wa Kampeni ya Chukua Hatua Dhidi ya
Umasikini 2015, iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
OFISA Habari Umoja wa Mataifa (UN), Bi. Usia Nkhoma Ledama amesema bado
lengo la kupunguza kiwango cha umasiki lililokuwa katika malengo ya
milenia yaliyomalizika mwakani litaendelea kuwa changamoto kwa nchi
mbalimbali kutokana na hali ya utekelezaji wake.
Bi.
Nkhoma ametoa ufafanuzi huo Uwanja wa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam
katika Uzinduzi wa Kampeni ya Chukua Hatua Dhidi ya Umasikini 2015
zilizozinduliwa leo Dar es Salaam.
Alisema jitihada zinafanyika na nchi mbalimbali zipo katika viwango
tofauti katika kulitimiza lengo hilo.
"...Kwanza
lazima tukubali kuwa ni lengo ambalo linachangamoto kubwa kiutekelezaji
karibia nchi nyingi, hivyo litaendelea kupewa uhimizaji kiutelekezaji
hata katika malengo yajayo," alisema Bi. Nkhoma.
Hata hivyo akizungumzia suala la kupunguza maambukizi ya Ukimwi alisema
bado ni lengo ambalo linachangamoto kubwa licha ya kwamba maambukizi
mapya bado yapo lakini nguvu kubwa imewekwa katika kupunguza hayo
maambukizi mapya.
"...Tupunguze
maambukizi mapya na tusiwe tena na watu wanaoendelea kufa kutokana na
maambukizi ya Ukimwi...hili bado ni lengo ambalo linaendelea kufanyiwa
kazi kwa nguvu kubwa pia linahitaji msukumo na jitihada za mtu mmoja
mmoja, lakini pia kama nchi, kama taifa na jumuiya za kimataifa katika
kupambana nalo," alisema.
Alisema
lengo la kupunguza vifo vya watoto wachanga na wajawazito bado ni lengo
lenye changamoto, hii ni kutokana na suala hili utekelezaji wake
unahitaji rasilimali ya kutosha kuhakiisha tuna hospitali, vituo vya
afya na klinii za kutosha kuhakikisha tuna sehemu za kutolea huduma kwa
akina mama na watoto.
Hospitali
zetu kuwa na vifaa na wahudumu wa afya waliosomea na kubobea kwenye
huduma hizo.
"Bado kuna changamoto lakini tutatumia changamoto zilizokuwa katika
utekelezaji kwa miaka iliyopita kutatua changamoto za sasa kimaboresho
zaidi. Kupunguza umasikini sio suala la sera bali ushiriki wa wananchi
mmoja mmoja oale alipo, pia hili ni suala mtambuka kutokana na
kutegemeana na sekta nyingine.
Mfano
mkulima hawezi kupunguza umasikini kama hana pembejeo, kama hana
miundombinu imara ya kusafirisha mazao yake kutoka shambani hadi sokoni
na pia kupata soko la uhakika anapoingiza mazao yake sokoni."
Alisema ili kupambana na hili inabidi kujengwa mazingira kuhakikisha
kila mmoja anashiriki kupambana na malengo hayo, mfano fursa za ajira na
fursa za kujiajiri haiwezekani kila mtu kuajiriwa so inabidi kuandaliwa
wengine kujiajiri wenyewe.
"...Sio
lazima kila mtu aajiriwe kila mtu anakipaji chake katika uzalishaji
kinaweza kutumika kwa kuendelezwa na kujikuta anafanya vizuri," alisema.
Kampeni ya Chukua Hatua Dhidi ya Umasikini 2015 zimezinduliwa rasmi leo
jijini Dar es Salaam na kushiriisha makundi mbalimbali, wazee, vijana,
wanafunzi wa Msingi na Sekondari, watu wenye ulemavu na makundi mengine
husika.
Post a Comment
HOME