RAIS KIKWETE MGENI RASMI MAADHIMISHO SIKU YA SHERIA
Jaji
Mkuu wa Tanzania Mh. Othman Chande (Kulia) akitoa ufafanuzi kwa
waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini mwaka
2015. Maadhimisho hayo yanaongozwa na maudhui yasemayo “ Fursa ya kupata
haki: wajibu wa Serikali, Mahakama na wadau”. Kushoto ni Mh. Hussein
Kattanga, Mtendaji Mkuu wa Mahakama.
Msajili
Mkuu wa Mahakama, Ignas Kitus (kulia) akizungumza akifafanua jambo
wakati Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Othman Chande alipokutana na waandishi
wa habari kuzungumzia maadhimisho ya Siku ya Sheria leo jijini Dar es
salaam.
Waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo leo. Picha na Aron Msigwa -MAELEZO.
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
Rais
Jakaya Kikwete anatarijiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha
maadhimisho ya Siku ya sheria nchini (Law Day) itakayofanyika Februari
4, 2015, katika viwanja vya mahakama vilivyopo mtaa wa Chimala jijini
Dar es salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Jaji Mkuu wa Tanzania
Mh. Othman Chande amesema kuwa maadhimisho hayo kwa mwaka huu
yanaongozwa na maudhui yasemayo “ Fursa ya kupata haki: wajibu wa
Serikali, Mahakama na wadau”.
Amesema
kwa mara ya kwanza maadhimisho hayo yataambatana na maonesho ya Wiki ya
Shera yatakayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja kuanzia
tarehe 30 Januari 2015 hadi tarehe 2 Februari 2015 .
Mh.Chande
ameeleza kuwa maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini na maonesho ya Wiki
ya Sheria yanaashiria mwanzo wa shughuli za mahakama kwa mwaka 2015 na
kufafanua kuwa kipaumbele kitatolewa katika kupunguza mrundikano wa
mashauri ya muda mrefu yaliyoko mahakamani na kushughulikia mashauri
yenye mvuto mkubwa kijamii,miradi mikubwa, uhujumu uchumi, madawa ya
kulevya, Biashara ndani na nje ya nchi na Rushwa.
Kuhusu
maonesho hayo amesema yanalenga kutoa elimu kwa wadau wa sheria na
huduma za kisheria kwa wananchi kuhusu Ufunguaji na uendeshaji wa
mashauri mbalimbali hasa mirathi, Utatuzi wa migogoro kwa njia ya
suluhu, kueleza mfumo mpya wa ulipaji wa tozo za kimahakama kwa njia ya
benki, Kutoa msaada wa kisheria, kutolewa vyeti vya mawakili, kupokea
maoni na malalamiko kwa ajili ya kuyatafutia ufumbuzi.
Ameeleza
kuwa wadau wakuu watakaoshiriki katika maonesho hayo ni Mahakama, Tume
ya Utumishi wa Mahakama, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi
ya Mkurugenzi wa Mashitaka, Chuo cha Uongozi wa Mahakama- Lushoto,
Taasisi ya Mafunzo ya Uansheria kwa vitendo Tanzania na Tume ya Haki za
Binadamu na Utawala Bora.
Wadau
wengine ni Taasisi zinazotoa msaada wa kisheria, TAKUKURU, Jeshi la
Polisi, Magereza, Chama cha Mawakili Tanganyika na Tume ya kurekebisha
sheria.
Amesema
pamoja na maonesho hayo kutakuwa na matembezi maalum ya kuadhimisha
Wiki ya Sheria tarehe 1 Februari 2015 yatakayoongozwa na Rais mstaafu wa
awamu ya pili Mh. Ali Hassan Mwinyi kuanzia Mahakama Kisutu kupitia
barabara za Serena-Ohio, Gymkana –Obama Road, Mahakama ya Biashara,
Barabara ya Kivukoni, Sokoine , Railway, Nkurumah, Lumumba na Mkunguni
hadi Mnazi Mmoja.
Post a Comment
HOME