0

Mkurugenzi Mkuu wa NHC atembelea miradi Geita na Mwanza

Msimamizi wa mradi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC Bombambili Geita Bw, Julius Ntoga (kulia) akitoa maelezo ya mradi huo kwa ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu alipotembelea mradi huo jana. Mradi huo wenye nyumba 48 ni wa nyumba za kuuza na unakamilika Februari mwaka huu.
Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC ukitembelea nyumba za gharama nafuu zilizojengwa eneo la Bombambili, Geita kwa ajili ya kuuzia wananchi.
Sehemu ya nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC eneo la Bombambili Mkoani Geita
Sehemu ya nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC eneo la Bombambili Mkoani Geita
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akitoa ufafanuzi kwa jopo la wasimamizi wa miradi ya Shirika na watendaji wengine ya namna wanavyoweza kupunguza gharama za ujenzi wa nyumba ili wananchi wengi wa kipato cha kati na chini waweze kumudu kuzinunua.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akiwapa mawaidha ya namna ya kupanua uwezo wa kikundi cha Vijana Kazi Wilayani Misungwi alipokitembelea jana. Kikundi hiki ni mojawapo ya vikundi vilivyopewa na NHC msaada wa mashine za kufyatulia matofali ya kufungamana ili kujiajiri. Bw. Mchechu ameziasa Halmashauri zote nchini kusaidia makundi ya vijana kwa kuwapa maeneo ya kufanyia kazi zao za kufyatua matofali na kuwapa tenda za ujenzi zinazokuwepo katika Halmashauri  hizo.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akionyeshwa na Afisa Ardhi wa Halmashauri ya Misungwi eneo lililotengwa na Halmashauri hiyo kwa ajili ya NHC kujenga nyumba za gharama nafuu
Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC ukionyeshwa ramani yenye eneo lililotengwa na Halmashauri ya Wilaya ya Nyamagana na Afisa Mipango Miji Bw. Maduhuna Bw. Ardhi Bw. Salvatory ili NHC iweze kujenga mji unaojitegemea(satellite town) na kuchochea ukuaji wa uchumi wa Jiji la Mwanza linalopakana na nchi za maziwa makuu.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akiwashauri viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyamagana kuona uwezekano wa kupunguza gharama ya NHC kulipa fidia ya eneo lililotengwa kujenga mji wa kisasa. Bw. Mchechu aliwataka viongozi hao kuitizama NHC kama chombo cha Serikali kinachowaletea maendeleo yao na si kama mwekezaji ili kufanya upangaji wa eneo hilo muhimu kufanyika.
Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC ukipokelewa katika mradi wa ujenzi wa nyumba eneo la Buswelu na Mkandarasi wa mradi huo Bw. Said Kiure(kulia)’
Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu ukipewa maelezo ya mradi wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu na Mkandarasi wa mradi huo Injinia Saidi Kiure walipotembelea mradi huo Jijini Mwanza jana. Suala la kupunguza gharama za ujenzi wa nyumba hizo ili ziwe nafuu lilisisitizwa na Mkurugenzi Mkuu.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akiendelea kutembezwa na Meneja wa NHC Mkoa wa Mwanza Bw. Benedict Kilimba katika mradi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC eneo la Buswelu.

Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu na ujumbe wake wakitembelea nyumba za NHC zilizoko barabara ya Kenyatta Jijini Mwanza ambazo zitaendelezwa ili kuongeza mapato ya Shirika na taswira ya Jiji hilo.

Post a Comment

HOME

 
Top