UNESCO YATAKA UBIA NA MWEDO
Mkurugenzi
Mtendaji wa asasi ya Maendeleo ya wanawake wa Kimasai (MWEDO), Ndinini
Kimesera (kushoto) akimkaribisha Mkurugenzi Mkazi wa Unesco nchini,
Zulmira Rodrigues kwenye ofisi za asasi hiyo kwa ajili ya mazungumzo
jijini Arusha.
Na Mwandishi Wetu, Arusha
SHIRIKA
la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni
(UNESCO) Tanzania, limesema kwamba litaingia ubia na asasi ya Maendeleo
ya wanawake wa Kimasai (MWEDO) ili kuimarisha mradi wa kijiji cha
digitali cha Ololosokwan.
Mradi
huo mkubwa unaoendeshwa na Unesco kwa kushirikiana na Samsung umelenga
kuinua maisha ya jamii ya wafugaji wa kimasai kwa kuwawezesha kielimu,
kitamaduni na kiujasirimali.
Kauli
ya kutaka kuingia ubia imetolewa na Mkurugenzi Mkazi wa Unesco nchini,
Zulmira Rodrigues wakati alipokutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Mwedo,
Ndinini Kimesera katika ofisi za Mwedo mkoani Arusha.
Alisema
Unesco inataka kutumia uzoefu wa Mwedo katika ushirikishaji wananchi
hasa katika uwezeshaji ujasirimali na elimu kufanikisha moja ya miradi
mikubwa ya kisayansi katika kijiji cha Ololosokwan.
Mkurugenzi
Mkazi wa Unesco nchini, Zulmira Rodrigues (kushoto) akiwa kwenye
mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya Maendeleo ya wanawake wa
Kimasai (MWEDO), Ndinini Kimesera (katikati) alipotembelea ofisi hizo
jijini Arusha. Kulia ni Mshauri wa kiufundi, usimamizi na tathmini wa
MWEDO, Bw. Paul Wilson.
Alisema
Rodrigues katika mazungumzo na Mtendaji wa Mwedo kwamba Unesco
imetambua haja ya kushirikisha wabia wengi katika maendeleo ili
kufanikisha mradi huo mkubwa unaotaka kutoa huduma za afya, elimu na
kuleta mabadiliko chanya katika jamii ya wafugaji wa kimasai ili kuweza
kutumia raslimali zao walizonazo kupata maendeleo ya kiuchumi na
kijamii.
Alisema
vifaa kwa ajili ya mradi wa kubadili kijiji cha Ololosokwan kuwa kijiji
cha digitali vimeshafika katika bandari ya Dar es salaam na wakati
wowote kuanzia wiki zijazo vitasafirishwa kuelekea kijiji hicho tayari
kwa utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa aina yake nchini ambao umelenga
moja kwa moja wahusika.
Alisema
mradi huo unataka kutumia teknolojia ya kisasa ya mawasiliano
kuwawezesha wananchi wa kijiji hicho kupata mabdiliko makubwa ya
kimaisha.
“Tumefika
kwenu kuona ni namna gani tutasaidiana kuimarisha mradi huu hasa utoaji
wa elimu na ujasirimali na utafutaji masoko” alisema.
Alisema
mradi huo umetaka kuhakikisha watoto wa wafugaji waume kwa wake
wanapata elimu kwa kupitia teknolojia ya kisasa, huku ujasirimali kama
utengenezaji wa shanga ukiwa katika soko na kuboreshwa zaidi.
Alisema kwa watu wazima wanataka kuwapa uelewa ili kuboresha maisha yao kiujasiriamali, kiafya na kiuchumi.
Alisema
soko la bidhaa za wanakijiji wa Ololosokwan kama urembo wa shanga na
mashuka zinazouzwa kwa watalii, zinaweza kupata soko zaidi kwa
kuboreshwa.
Afisa
Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la
Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Bw. Al Amin Yusuph (kulia)
akifafanua jambo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya Maendeleo ya
wanawake wa Kimasai (MWEDO), Ndinini Kimesera (hayupo pichani). Kulia
ni Mshauri wa kiufundi, usimamizi na tathmini wa MWEDO, Bw. Paul Wilson.
Alisema
ameridhika na uhodari uliooneshwa na Mwedo katika ujasiriamali na hivyo
wanataka kuimarisha uhusiano huo kwa kuhakikisha inawaleta watu wa
kusaidia kuboresha elimu ya utengenezaji wa vifaa hivyo kwa soko la
mataifa.
Alisema kwamba pamoja na kuwataka Mwedo kutafuta hosteli kwa ajili ya
wabunifu hao ili kuziongeza thamani bidhaa kwa soko la kimataifa.
Naye Mtendaji wa Mwedo amesema kwamba wapo tayari kushirikiana na Unesco katika miradi ya wananchi wa jamii ya wafugaji.
Mkurugenzi
Mkazi wa UNESCO aliambatana na Afisa mipango ya Elimu wa Shirika la
UNESCO, Bi. Jennifer Kotta (kulia) pamoja na Afisa Miradi ya
Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (kushoto).
Katikati ni Afisa Mradi wa MWEDO, Martha Sengeruan.
Mkurugenzi
Mkazi wa Unesco nchini, Zulmira Rodrigues akiangalia bidhaa mbalimbali
zinazotengenezwa na wakinamama wa kimasai kwenye duka la MWEDO mara
baada ya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya Maendeleo ya
wanawake wa Kimasai (MWEDO), Ndinini Kimesera (kulia). Katikati ni
Afisa mipango ya Elimu wa Shirika la UNESCO, Bi. Jennifer Kotta.
Mkurugenzi
Mkazi wa Unesco nchini, Zulmira Rodrigues (kulia) akiteta jambo na
Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya Maendeleo ya wanawake wa Kimasai
(MWEDO), Ndinini Kimesera mara baada ya mazungumzo.
Post a Comment
HOME