Kauli ya Waziri Chikawe kuhusiana na Waganga wanaochangia mauaji ya Albino
Matukio ya kuuawa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi ‘Albino’ bado yameonekana kuendelea kuchukua nafasi hasa katika Mikoa ya kanda ya Ziwa hali inayozidi kutishia amani ndani ya familia nyingi.
Waziri wa mambo ya ndani Mathias Chikawe ametoa tamko kuwa kutakua na operesheni ya kitaifa ya kuwasaka na kuwakamata waganga wa kienyeji maarufu kama wapiga ramli ili kuwafikisha mahakamani.
Uamuzi wa Waziri huyo unatokana na kukithiri kwa vitendo vya unyanyasaji wa watu wenye ulemavu vikishika kazi kutokana na kuuawa kwa imani za kishirikina.
Chikawe alisema watashirikiana na Chama cha watu wenye ulemavu TAS kuwabaini wahalifu na kuwachukulia hatua ili kupunguza vitendo hivyo.
Post a Comment
HOME