RAIS KIKWETE AHANI MSIBA WA MFALME WA SAUDI ARABIA, AWASILI BERLIN, UJERUMANI, KWA ZIARA YA KIKAZI JANUARY 26, 2015
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa mkono wa pole kwa watawala na familia mjini Riyadh, Saudi Arabia Jumapili, Januari 25, 2015, alipofika kuhani kuhani kifo cha Mfalme Abdullah bin Abdul Aziz al Saud aliyefariki Alhamisi na kuzikwa Ijumaa ya wiki iliyopita. Baada ya kuhani msiba wa Mfalme Abdullah, Rais Kikwete ameendelea na safari yake kwenda nchi za Ujerumani na Ufaransa kwa ziara za kikazi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Bi Fawzia Rasheed, Mkuu wa Sera wa Global Alliance for Vaccines and Immunization (Gavi Alliance) alipotua mjini Berlin, Ujerumani, January 26, 2015 kuungana na viongozi mbali mbali duniani kujadili jinsi ya kuboresha mipango ya utoaji chanjo kwa watoto wadogo hasa katika nchi zinazoendelea.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, akiwasili katika Uwanja wa Ndege wan Kijeshi mjini Riyadh, Saudi Arabia, Januari 25, kuhani kifo cha Mfalme Abdullah bin Abdul Aziz al Saud aliyefariki January 22, 2015 na kuzikwa January 23, 2015 . Baada ya kuhani msiba wa Mfalme Abdullah, Rais Kikwete ataendelea na safari yake kwenda nchi za Ujerumani na Ufaransa kwa ziara za kikazi.
Post a Comment
HOME