Mtuhumiwa sugu wa ujambazi katika mikoa ya Mwanza,Shinyanga na Simiyu atiwa mbaroni
Kamanda
wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga,SACP Charles Mkumbo akionesha
silaha iliyokuwa ikitumiwa katika harakati za matukio ya ujambazi katika
kijiji cha Idukilo Kata ya Luhumbo Mwadui wilayani Kishapu Mkoa wa
Shinyanga.Kushoto ni Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza,SACP
Valentino Mlowola na kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu,SACP
Justus Kamugisha.
Kamanda
wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga SCP Charles Mkumbo akionesha nguo
ambazo zilikutwa kwa Mtuhumiwa kiongozi huyo wa genge la uhalifu ambazo
zinasemekana ni za baadhi ya watu waliouawa wakiwemo majambazi aliokuwa
akishirikiana nao ambao aliwauwa kwa maslahi yake.
"Hii ni mifupa tuliyoikuta nyumbani kwa mtuhumiwa".
Kamanda
wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza,SACP Valentino Mlowola akiwa na
makamanda wenzake SACP Charles Mkumbo (Shinyanga) na SACP Justus
Kamugisha (Simiyu) wakati wakizungumza na waandishi wa habari kufuatia
kutiwa mbaroni kwa mtuhumiwa wa ujambazi ambaye pia ni mfanyabiashara
aitwaye Njile Samweli (46) marufu kwa “John” wa mjini Bariadi mkoani
Simiyu, aliyekuwa akifanya matukio ya uhalifu katika Mikoa ya Mwanza,
Simiyu, Shinyanga, Singida na Tabora.
Sehemu ya vitu vilivyokutwa kwa mtuhumiwa huyo.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Simiyu,SACP Justus Kamugisha akiwasilisha taarifa kwa waandishi wa habari.
PICHA NA HABARI NI KWA HISANI YA GSENGO BLOG.
JESHI
la Polisi limefanikiwa kumtia mbaroni mtuhumiwa wa ujambazi ambaye pia
ni mfanyabiashara aitwaye Njile Samweli (46) marufu kwa “John” wa mjini
Bariadi mkoani Simiyu, aliyekuwa akifanya matukio ya uhalifu katika
Mikoa ya Mwanza, Simiyu, Shinyanga, Singida na Tabora.
Wakizungumza
na waandishi wa Habari jijini Mwanza, Makamanda wa Polisi SACP
Valentino Mlowola (Mwanza),SACP Charles Mkumbo (Shinyanga) na SACP
Justus Kamugisha (Simiyu), walisema kuwa mtuhumiwa huyo ambaye ni
mfanyabiashara wa mjini Bariadi mkazi wa kijiji cha Lyoma alikamatwa
Januari 5 mwaka huu wilayani Bariadi Mkoa wa Simiyu.
Kamanda
Mlowola alieleza kuwa kukamatwa kwa kiongozi huyo hatari wa kundi la
ujambazi katika mikoa hiyo kumetokana na kukamatwa kwa mmoja wa
washirika wa kundi lake Januari 5 jijini Mwanza kutokana na taarifa za
siri kutoka kwa raia wema waliotoa kwa Jeshi la Polisi,hali iliyopelekea
kuundwa kikosi kazi kushirikisha mikoa hiyo cha kufatilia mtandao huo
na kufanikiwa kuwakamata.
Aliwataja
watuhumiwa waliokamatwa kuwa ni Mabula Lyanga (36) maarufu kwa jina la
Magana mkazi wa kijiji cha Bugarama wilayani Maswa Mkoa wa Simiyu akiwa
na jeraha la kupigwa risasi na jambazi mwenzake aitwaye Njele (Kiongozi
wa kundi) kwenye bega lake la kulia kutokana na raia wema kumtilia
mashaka na kuanza kumfatilia na kunaswa na polisi.
“Baada
ya kumkamata mtuhumiwa huyu wa ujambazi katika mahojiano na askari wetu
alimtaja mtuhumiwa mwenzake Njile kupiga risasi wakiwa katika harakati
za tukio la ujambazi wa kutumia silaha katika kijiji cha Idukilo Kata ya
Luhumbo Mwadui wilayani Kishapu Mkoa wa Shinyanga Januari 5 mwaka
huu,”alieleza.
Kamanda
Mlowola alisema kuwa watuhumiwa hawa baada ya kufanya uhalifu huo na
uporaji na kutofautiana na kiongozi wake Njile,alimfyatulia risasi mbili
na kumjeruhi kwenye bega, tuliwatuma askari wa Idara ya Upelelezi
kutoka Mwanza kwenda kufatilia na kufanya msako mkali kwa kushirikiana
na wenzao wa Bariadi mkoani Simiyu.
“
Kikosi kazi chetu kilifanikiwa kumkamata Njile na katika mahojiano naye
binafisi alikiri kuhusika na tukio hilo na kuelezea kufanya matukio
mengine mengi katika Mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Singida na
Tabora ikiwemo kuwauwa washirika wenzake na kuwataja wengine ikiwemo
alipokuwa amehifadhi silaha (SMG) risasi 331 na Magazine tisa
vilivyotumika,”alisema.
SACP
Mlowola alitaja matukio kadha waliyofanya watuhumiwa hao katika Mkoa wa
Mwanza kuwa ni pamoja na kuvamia na kupora fedha kiasi cha Sh milioni
3,500,000/= katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Samba katika Kisiwa
cha Bulubi wilayani Ukerewe Agosti mwaka 2014, Oktoba 2 mwaka 2014
katika Kijiji cha Mahaha walivamia maduka kadhaa na kupora fedha kiasi
cha Sh milioni 3 na Pikipiki moja na kumuua mtu mmoja.
Tukio
jingine lilifanyika Oktoba 2014 eneo la Malya wilayani Ngudu ambapo
walivamia na kupora fedha kiasi cha Sh milioni 2 na kumjeruhi mtu mmoja
na wahusika wa matukio yote hayo walioshiriki ni Njile (kiongozi),
Lyagwa (aliyepigwa risasi na Njile), Magingi Doto “Kafuru”,Thomas,
Daniel Pastory, Mashauri Ngulyati, Kipisto Chenya.
Naye
Kamanda SACP Mkumbo ( Simiyu), alisema kwamba baada ya kikosi kazi
kufanya ufatiliaji kutokana na maelezo ya mtuhumiwa Njile walifanikiwa
kukamata bunduki moja ya kivita (SMG) yenye namba BP 3402, risasi 331,
Magazine tisa, mifupa na nguo zinazosadikiwa kuwa ya marehemu
waliouwawa na mtuhumiwa huyo.
Alisema
mtuhumiwa huyo na washirika wake waliafanya matukio mengine ya uhalifu
katika wilaya ya Itilima ,Maswa, Meatu ,Bariadi ambapo walipora Sh.20.5
milioni.
Kamanda
wa Polisi Mkoani Shinyanga, SACP Kamugisha,alisema watuhumiwa hao
walifanya uhalifu katika wilaya ya Kishapu walikopora Sh.3.2 na simu
aina ya Nokia pia walimjeruhi mwenzao (Mabula Lyagwa) kwa risasi kabla
ya kumbeba na kumtelekeza mjini Maswa.
Alisema
walifanya matukio mengine katika wilaya ya Igunga,kwa kupora simu na
fedha,pia walipora mkoani Singida kiasai cha Sh.1.5 na hadi sasa jeshi
hilo linawashikilia watuhumiwa watano na wengine bado wanatafutwa, mara
baada ya taratibu kukamilika watafikishwa mahakamani.
Post a Comment
HOME