NGO's YA APEC KWA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI DODOMA YAFUNGA MAFUZO KWA WAENDESHA PIKIPIKI (BODABODA) MKOANI HUMO
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma,SACP David Misime akiongea katika kufunga mafuzo
kwa waendesha pikipiki (Bodaboda) wa Manispaa ya Dodoma yaliyoendeshwa
na Shirika lisilo la kiserikali la –APEC - kwa kushirikiana na Jeshi la
Polisi.
Muwakilishi wa Waendesha Pikipiki (Bodaboda) Mkoa wa Dodoma, Bw. Erasto Kasugu akisoma risala kwa mgeni rasmi,wakati wa kufunga mafuzo
kwa waendesha pikipiki (Bodaboda) wa Manispaa ya Dodoma yaliyoendeshwa
na Shirika lisilo la kiserikali la –APEC - kwa kushirikiana na Jeshi la
Polisi..
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la kiserikali la APEC Bw. Respicius Timanywa akiongea jambo kwenye ufungaji wa mafunzo hayo
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma,SACP David Misime akikabidhiwa zawadi na waendesha pikipiki(Bodaboda).
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma,SACP David Misime akikabidhi vyeti vya mafunzo kwa washiriki.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo wakisikiliza.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma,SACP David Misime akiwa katika picha ya pamoja na wakufunzi toka Jeshi la Polisi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma,SACP David Misime akiwa katika picha ya pamoja na wakufunzi wa shirika la APEC.
Na. Sylvester Onesmo wa
Jeshi la Polisi Dodoma.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishina Msaidizi
Mwandamizi wa Polisi,SACP David Misime amesema Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma
kwa kushirikiana na wadau wengine litaendeleza msako kwa wale wote waendesha
pikipiki ambao hawana leseni kwani walishapewa muda mrefu ili waweze kupata leseni pamoja na mafunzo ya udereva.
Ameyasema hayo wakati wa kufunga mafuzo kwa waendesha
pikipiki (Bodaboda) wa Manispaa ya Dodoma yaliyoendeshwa na Shirika
lisilo la kiserikali la –APEC - kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi,mafunzo
yaliyochukua wiki moja kuanzia tarehe 12/01/2015 hadi tarehe 19/01/2015.
Kamanda Misime amesema elimu waliyoipata waendesha pikipiki
(bodaboda) waitumie vizuri ili kujiepusha na ajali ambazo kwa kiwango kikubwa
zinasababishwa na makosa ya kibinadamu na ukosefu wa mafunzo.
Aidha Kamanda Misime ameeleza kuwa takwimu za kuanzia mwezi
Januari hadi Desemba 2014 zinaonyesha ajali za pikipiki zilifikia 62, kati ya
hizo ajali za vifo ni 16 ambazo zilisababisha vifo vya watu 18. Pia ajali za
majeruhi zilikua 28 na jumla ya watu 31 walipata majeraha sehemumbalimbali.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Ant – Poverty and Development Care
(APEC) Bw. Respicius Timanywa amesema kutokaa na ajali za barabarani kuwa
nyingi hapa nchini, imebainika kuwa ajali nyingi za vifo na majeruhi ni za
waendesha pikipiki wasio na mafunzo stahiki na utafiti uliofanywa na APEC kwa
Mkoa wa Dodoma, umebaini kuwa waendesha pikipiki wengi kutokuwa na elimu ya
usalama barabarani, leseni za udereva na kutokuwepo na mahusiano mazuri kati
yao na Jeshi la Polisi jambo linalosababisha ongezeko la ajali za barabarani na
vurugu.
Pia amezitaja changamoto mbalimbali zilizopo katika kazi ya
APEC ni muitikio mdogo wa walengwa ambao ni madereva wa vyombo vya moto,
madereva wenye leseni bila vyeti vya kutoshiriki mafunzo katika vyuo
mbalimbali.
Akisoma risala kwa mgeni rasmi kwa niaba ya Katibu wa
waendesha pikipiki (Bodaboda) Manispaa ya Dodoma Bw. Erasto Kasugu amesema katika mafuzo haya waendesha pikipiki wapatao 193 kutoka maeneo mbalimbali katika Manispaa ya
Dodoma wamepatiwa mafunzo ya usalama barabarani na pia walieleza changamoto
zinazowakabili ambazo ni kukabwa na kuibiwa pikipiki, madereva wa magari
makubwa hususani malori kutowathamini waendesha pikipiki wanapokuwa barabarani,
baadhi ya abilia kukataa kuvaa helmet, baadhi ya waendesha pikipiki kuvaa jina
la bodaboda huku wakifanya vitendo vya uhalifu pamoja na baadhi ya waendesha
pikipiki kukataa kushiriki mafunzo ya usalama barabarani kama yaliyotolewa na
APEC.
Aidha wamesema kwa kuwa wamepata mafunzo ya Polisi Jamii na
mbinu za kuwakamata waalifu, wameomba ushirikiano mkubwa pindi wanapotoa
taarifa za matukio yasiyofaa baada ya kuwatilia shaka au kuwabaini waarifu.
Post a Comment
HOME