Naibu waziri wa maliasili na utalii awataka vijana kujituma kufanya kazi
Naibu waziri wa maliasili na utalii Mahmoud Mgimwa ambaye ni mbunge wa jimbo la mufindi kusini akiwa katika moja ya ziara zake za wizara ya maliasili na utalii
Naibu waziri wa maliasili na utalii Mahmoud Mgimwa ambaye
ni mbunge wa jimbo la mufindi kusini akiwa katika moja ya ziara zake za
wizara ya maliasili na utalii na wengine ni viongozi wa TANAPA
Naibu waziri wa maliasili na utalii Mahmoud Mgimwa ambaye ni mbunge wa jimbo la mufindi kusini akiwa ziarani
na Fredy Mgunda ,Iringa
Naibu
waziri wa maliasili na utalii,Mahmoud Mgimwa ambaye ni mbunge wa jimbo
la mufindi kusini amewataka vijana kujituma na kutumia fursa mbalimbali
ambazo zinatolewa na serikali.
Akizungumza na mtandao huu,Mgimwa alisema kuwa vijana wengi wamekuwa wakibweteka kwa kutojituma kufanya kazi na kuendelea kuilaumu serikali.
“Eti
asubuhi unawakuta vijana wamekaa kwenye vijiwe wakizungumza siasa na
kucheza mabao wakati hawajui mchana watakula wapi na jioni watarudi na
nini nyumbani”alisema Mahmoud Mgimwa.
Mgimwa
ameendelea kuwaomba vijana wengi wenye fursa ya kurudi au kuingia
shuleni upya warudi kwa kuwa dunia ya sasa inataka wasomi wengi kutokana
na mabadiliko ya kiuchumi na sayansi na teknolojia na ndio sababu
inayopelekea hata watu wazima kurudi shuleni.
“Vijana
mnatakiwa kujifunza kutoka kwa watu wazima ambavyo wamekuwa wakijituma
kufanya kazi kwa bidii na kujituma ilimradi kuwatengenezea watoto maisha
mazuri pamoja na kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla”alisema Mahmoud Mgimwa.
Wakati huo huo Naibu waziri Mgimwa amewataka
wakinamama kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali katika
uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi wa kumi mwaka huu.
Mgimwa
ameeleza kuwa wanawake waondoe hofu ya kugombea hasa kukiwa na
ushindani wa wagombea wanaume kwa kuogopa kuchafuliwa kwa mambo
yasiyokuwepo.
Ameendelea
kusema kuwa wananchi wasishawishiwe na propaganda za wanasiasa na
badala yake wachague viongozi bora wenye uwezo wa kuongoza kutoka katika
chama chochote.
Aidha
ameongeza kuwa viongozi wawe na sera za kutekelezeka ili kuwatendea
haki wapiga kura wao hali itakayowafanya waaminike katika jamii.
Mbali
na hayo Mgimwa amewakumbusha vijana kutokubali kutumiwa na baadhi ya
wanasiasa katika kuleta vurugu hasa katika kipindi hiki cha kuelekea
uchaguzi mkuu na badala yake wachague kiongozi mwenye weredi na sifa za
kuwa kiongozi kutokana na sera za chama chake.
Ameendelea
kusema kuwa vijana wajitokeze kwa wingi katika kupiga kura ndiyo katika
katiba iliyopendekezwa ili kuweza kufanya uchaguzi ulio wa haki na
amani pia kujitokeza katika kujiandikisha katika daftari la wapiga kura
pamoja na kupiga kura.
Amemaliza
kwa kuwataka wananchi wa jimbo la mufindi kusini kuwa na imani nae kwa
kuwa amefanya yote ambayo aliwaahidi katika uchaguzi wa mwaka wa 2010 na
amewaomba waendelee kuwa na imani naye katika kutekeleza mambo mapya
ambayo wamejitokeza kwa lengo la kuleta maendeleo ya jimbo hilo.
Post a Comment
HOME