ZIARA YA WAZIRI NYALANDU MJINI RIADH, SAUDI ARABIA
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akiwa katika mazungumzo
na Mwana Mfalme wa Saudia, Prince Bandar bin Saud bin Mohammad Al-Saud,
kuhusiana na masuala ya uhifadhi, mjini Riyadhi, jana. Wengine ni ujumbe
uliofuatana na Lembeli, ni Katibu Mkuu Wizara hiyo Dk. Adelhem Meru,
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James
Lembeli na Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii, Mchungaji Peter Msigwa,
muda mfupi kabla ya kuanza kwa mazungumzo baina ya Tanzania na Saudi
Arabia jijini Riyadh, Saudi Arabia.
KATIBU
Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Adelhem Meru (katikati),
akizungumza kwenye mkutano baina ya ujumbe wa Tanzania na Saudi Arabia.
Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira,
James Lembeli na Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Profesa
Abdillah Omari.
UJUMBE
wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro
Nyalandu, wakiwa kwenye picha ya pamoja na zawadi waliyopewa na Mwana
Mfalme Prince Bandar bin Saud bin Mohammad Al-Saud, ambaye pia ni Rais
wa Mamlaka ya Wanyamapori ya Saudi Arabia. Wengine kutoka kulia ni
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dk. Adelhem Meru; Balozi wa
Tanzania Saudi Arabia, Profesa Abdillah Omari; Mwenyekiti wa Kamati ya
Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli; Waziri Kivuli wa
Maliasili na Utalii, Peter Msigwa; Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan
Kijazi na Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Herman Keraryo.
Prince
Bandar bin Saud bin Mohammad Al-Saud, ambaye pia ni Rais wa Mamlaka ya
Wanyamapori ya Saudi Arabia, akizungumza wakati wa mkutano huo. Pembeni
ni Waziri Nyalandu.
Post a Comment
HOME