Waziri Mukangara apokea msaada wa vifaa vya michezo kutoka kwa Serikali ya China
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB)
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kukabibidhiwa
msaada wa vifaa vya michezo kutoka Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China leo jijini Dar es
Salaam.Kutoka kushoto ni Balozi wa China hapo nchini Lu Youqing na Mwakilishi Mkuu wa
Wafanyabiashara kutoka China waishio nchini Lin Zhiyong. Jumla ya vifaa kumi na nne
vimetolewa ambavyo ni Roboti ya kujifunzia mpira wa Meza, Kifaa cha kupimia upepo kwa ajili
ya Riadha,Nyavu ya mpira wa Meza, Mashine ya kupimia Uzito,Ulingo wa
Ngumi,Kompyuta,Printa, Radio Call, mashine ya kutafsirina kuhesabu matokeo katika riadha na
nyaya za umeme vyenye thamani zaidi ya 200.
Balozi wa China hapa nchini Lu Youqing akizungumza na waandishi wa habari (hawapo
pichani) wakati wa hafla ya kukabibidhi msaada wa vifaa vya michezo kwa Serikali ya Tanzania
vilivyopokelewa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara
(hayupo pichani) leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB)
akicheza Mpira wa Meza na Balozi wa China hapa nchini Lu Youqing (kulia) wakati wa hafla ya
kukabibidhiwa msaada wa vifaa vya michezo kutoka Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China leo
jijini Dar es Salaam.
Balozi wa China hapa nchini Lu Youqing akielezea namna mmtambo wa Radio Call
unavyofanya kazi, katika mwenye blauzi ya kitenge Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Dkt. Fenella Mukangara, na Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo Bibi.
Juliana Yassoda.
Ulingo wa kisasa uliokabidhiwa kwa Serikali ya Tanzania kutoka Serikali ya Jamhuri ya
Watu wa China leo jini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB)
akibadilishana hati ya makabidhiano ya vifaa vya michezo na Balozi wa China hapa nchini Lu
Youqing (kulia) wakati wa hafla ya kukabibidhiana vifaa hivyo leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Frank Shija.
Na Benjamin Sawe,
WHVUM
Serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imepokea msaada wa vifaa
mbalimbali vya mchezo wa ngumi na riadha kutoka kwa Serikali ya Watu wa China vyenye
jumla ya thamani ya zaidi ya shilingi milioni 200.
Akizungumza katika makabidhiano hayo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dr.
Fennela Mukangara alisema msaada huo ni sehemu ya kuboresha tasnia ya michezo ikiwa ni
pamoja na kuendeleza ushirikiano wa muda mrefu baina ya nchi hizo mbili.
“Msaada huu ni kiashirio tosha kwa wananchi wa nchi zote mbili na umekuwepo ukiendelea
kuimarika na tunazo fursa za kuendeleza ushirikiano huu kwa manufaa ya wananchi
wetu”.Alisema Mheshimiwa Mukangara.
Aidha alimuhakikishia Mheshimiwa Balozi wa China kuwa Watanzania wanathamini mchango
mkubwa wenye lengo la kuendeleza michezo hapa nchini kwani China na Tanzania zina historia
ya pamoja ya takribani ya miaka 50 mpaka sasa.
Alisema kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa imewasilisha kwenye
ofisi ya Ubalozi wa China mapendekezo ya kuendeleza ushirikiano kupitia sekta ya michezo
ambapo matumaini yake ni kuwa kwa kupitia maeneo hayo zitapatikana fursa zaidi kwa vijana
kuendeleza ushirikiano baina ya nchi mbili kupitia michezo ikiwa ni pamoja na kujifinza
mambo muhimu katika tasnia ya Michezo.
Akizungumza katika makabidhiano hayo Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China Mh. Lu
Youqing alisema Serikali yake itaendelea kuwa na ushirikiano na Serikali ya Tanzania katika
sekta mbalimbali ikiwa ni ishara ya kudumisha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.
Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na “Table Tennis 2”, Wind Speed Gage Device 2, “UPS 1, Table
Tennis Net” 7, “Electronic Weigher 2”, Computer 1, “Table Tennis Balls”, “Boxing Ring 2”,
“Table Tennis 5”, “Printer 1”, “Electronic Cable 6”, “Radio Call 2”, “Anemograph 2”, na
Electric Timing and Scoring Interpretation Device For Finishing line 1” ambapo jumla yake ni
zaidi ya shilingi milioni 200.
Mpaka sasa Serikali ya China imeshaipatia msaada Serikali ya Tanzania jumla ya shilingi
bilioni moja ili kuendeleza sekta mbalimbali nchini.
Post a Comment
HOME