UFAHAMU MTANDAO WA MALEZI MAKUZI NA MAENDELEO YA WATOTO WADOGO TANZANIA (TECDEN)
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Bruno Ghumpi |
Mtandao
wa Malezi Makuzi na Maendeleo ya Watoto Wadogo Tanzania – TECDEN ni
chombo kinachoundwa na mashirikia mbalimbali yanayofanya kazi za
kuhudumia watoto wadogo Tanzania.
Mtandao huu ulianzishwa mwaka 2000 na kusajiliwa rasmi mwaka 2004. Makao makuu ya Mtandao huu yapo Jijini Dar es salaam.
Hadi
kufikia mwaka 2014 Mtandao huu una jumla ya mashirika wanachama
wasiopungua 200 katika mikoa 14 ya Tanzania bara na Visiwani yanayotoa
huduma kwa watoto wadogo Tanzania
Lengo kuu la Mtandao ni kuboresha huduma za watoto wadogo Tanzania ili
waweze kukua na kufikia utimilifu wao
Shughuli Kuu za Mtandao ni pamoja na:-
• Kufanya ushawishi na utetezi wa masuala yanayohusu uboreshaji wa
huduma na kulinda haki za watoto wadogo ikiwa ni pamoja na kushawishi
maboresho ya sera na kufuatilia utekelezaji wa sheria na miongozo
mbalimbali inayohusu uboreshaji wa huduma kwa watoto wadogo Tanzania.
• Kuhamasisha jamii na watoa huduma kutambua umuhimu wa kuimarisha na
kuwezesha watoto wadogo kupata mahitaji na haki zao za msingi.
• Kuimarisha mifumo ya upashanaji habari na kuelimishana katika ngazi
zote za huduma kwa watoto wadogo.
• Kutafiti na kutumia matokeo ya utafiti katika kushauri uboreshaji wa
huduma kwa watoto wadogo Tanzania.
Dhana
ya Malezi Makuzi na Mendeleo ya Awali ya Mtoto (MMMAM)
Malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto ni istilahi ya jumla ya
programu na vitendo vinavyoandaliwa kuwasaidia watoto (kuanzia mimba,
kuzaliwa hadi miaka 8) ili kukua vizuri kimwili, kiakili, kijamii,
kihisia, kimaadili na kiroho.
Watoto
wanahitaji kuchangamshwa katika nyaja na hatua zote za ukuaji, kiakili
kwa michezo, kujifunza kuzungumza, kukaa, kutambaa, kutembea na kupatiwa
fursa ya kuanza kujifunza mambo mbalimbali pamoja na utamaduni wao.
Utoaji
wa huduma jumui za MMMAM.
Huduma hizi hujumuishwa ili kuwawezesha watoto wengi kupata huduma
jumuishi za MMMAM zitolewazo na sekta mbali mbali katika mkabala jumui.
Huduma hizi zinapaswa kupatikana kuanzia ngazi ya familia ,vituo vya
afya ya msingi,vituo vya kulelea watoto mchana, vituo vya Malezi Makuzi
ya awali ya mtoto vinavyomilikiwa na Jamii, madarasa ya awali na
madarasa ya msingi hususani darasa la kwanza na la pili.
Katika
kutekeleza shughuli zake Mtandao wa TECDEN umekuwa ukishirikiana na
mashirika mbalimbali ya wabia wa maendeleo ikiwemo shirika la Children
in Crossfire kutoka nchini Ireland na shirika la Better Way Foundation
kutoka nchini Marekani.
Ili
kujua habari zaidi za TECDEN na masuala ya utoaji huduma kwa watoto
wadogo na faida zake, unaweza kutembelea ofisi ya Mtandao makao makuu
iliyopo Jengo la Posta mkabala na Wizara ya Mambo ya Ndani Nchi na Makao
Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam.
Unaweza
pia kuwasiliana kwa njia ya simu au barua pepe na Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji Ndugu Bruno Ghumpi kwa namba 0754 690 556 na barua pepe ecdnetwork@gmail.com na ghumpibr@yahoo.com
Post a Comment
HOME