RAIS MSTAAFU WA BOTSWANA MH. FESTUS MOGAE ATEMBELEA TAASISI YA UONGOZI
Rais
mstaafu wa Botswana Mh. Festus Mogae (kushoto) akipokelewa na Afisa
Mtendaji Mkuu wa UONGOZI Institute Profesa Joseph Semboja pale kiongozi
huyo mstaafu alipotembelea ofisi hiyo iliyo chini ya Ofisi ya Rais jana
Masaki, jijini Dar es Salaam.
Rais
mstaafu wa Botswana Mh. Festus Mogae akisaini kitabu cha wageni katika
ofisi za UONGOZI Institute pale alipofika kwenye taasisi hiyo kufahamu
zaidi kuhusu maendeleo yake. Anayeshuhudia kushoto ni Afisa Mtendaji
Mkuu wa UONGOZI Institute Profesa Joseph Semboja na Mkuu wa Idara ya
Sera na Utafiti wa taasisi hiyo Bw. Dennis Rweyemamu.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa UONGOZI Institute Profesa Joseph Semboja (wa pili
kushoto) akimuelezea Rais mstaafu wa Botswana Mh. Festus Mogae (kulia)
kuhusu mradi wa ujenzi wa taasisi ya mafunzo ya UONGOZI Institute
unaoendelea katika mji wa Bagamoyo, Pwani. Kutoka kulia ni Dr. Linda
Ezekiel Mkurugenzi wa Sekta za Kijamii kutoka Presidential Delivery
Bureau (PDB) na Mkuu wa Sera na Utafiti wa UONGOZI Institute Bw. Dennis
Rweyemamu.
Rais
mstaafu wa Botswana Mh. Festus Mogae pia alipata wasaa wa kuzungumza na
wafanyakazi wa UONGOZI Institute, kuelezea kuhusu uzoefu wake katika
uongozi, utumishi wa umma, pamoja na maono yake kwa bara la Afrika na
watu wake.
Rais
mstaafu wa Botswana Mh. Festus Mogae akizungumza na wafanyakazi wa
UONGOZI Institute (hawapo pichani) taasisi inayojishughulisha na utoaji
mafunzo ya uongozi kwa viongozi serikalini pamoja na utafiti na ushauri
wa kisera unaoweza kuleta maendeleo endelevu nchini. Pembeni yake ni
Afisa Mtendaji Mkuu wa UONGOZI Institute Profesa Joseph Semboja.
Rais
mstaafu wa Botswana Mh. Festus Mogae (aliyeketi kulia) na mwenyeji wake
Afisa Mtendaji Mkuu wa UONGOZI Institute Profesa Joseph Semboja
(aliyeketi kushoto) katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa UONGOZI
Institute jana jijini Dar es Salaam.
Post a Comment
HOME