0

BENKI MPYA YA MAENDELEO YA KILIMO(TADB) YAAHIDI KUTOA HUDUMA BORA ZA KIBENKI KWA WATEJA WAKE

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Thomas Samkyi akizungumza katika warsha juu ya kujadili mpango wa maendeleo wa taasisi hiyo kwa miaka 25 ijayo. Warsha hiyo ilifanyika hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency, Dar es Salaam.
Mkuu wa Mipango, Sera na Ushirikiano wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania, Francis Assenga akizungumza na wadau katika mkutano huo.
Wadau wa sekta ya kilimo, uvuvi na ufugaji wakifuatilia warsha ya mpango wa maendeleo wa miaka 25 wa benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) uliofanyika kwenye hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency, Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Sophia Kaduma akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi, wakurugenzi wa benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania pamoja na wadau walioshiriki warsha ya Maendeleo ya miaka 25.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Sophia Kaduma (katikati) waliokaa akiwa na Viongozi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) mara baada ya kufungua mkutano wa Mpango wa Maendeleo wa miaka 25 ya benki hiyo.

Na Bakari Issa,Globu ya Jamii - Dar

Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini (TADB) imeahidi kutoa huduma bora za kibenki kwa wateja wake ili kuwa na mwanzo mzuri wa kutoa huduma bora za kifedha kwa wananchi.

Benki hiyo ya Maendeleo ya Kilimo imeanza na mtaji wa Sh 100 Billion kwa mwaka 2015-2016 na kuahidi kutenga kiasi hicho hicho cha Sh 100 Billion kila mwaka kwa ajili ya maendeleo ya kibenki.

Akizungumza katika warsha fupi iliyofanyika leo katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam,Mjumbe wa Bodi ya TADP,Adrew Temu amesema  wanataka kuanza na mwanzo mzuri wa kutoa huduma bora za kibenki kwa wananchi na kusema kuwa benki hiyo sio tu ya watu wa tabaka la juu bali itawahusu hata watu wa tabaka la kati,chini,wazalishaji,wasindikaji katika sekta ya kilimo.

Aidha,Bw.Temu amesema wataendelea kuwaelimisha wananchi juu ya huduma za kibenki ya kilimo na kuahidi watakayoyatasmini watatekeleza na kutoa msimamo katika tija kwa pamoja na kutoa huduma nafuu za kifedha.

Kwa upande wake,Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na Chakula,Sophia Kaduma amesisitiza juu ya umuhimu wa kupanga mikakati na kuweka vipao mbele kwa kuhakikisha mikakati pamoja na vipao mbele hivyo vinasimamiwa na kuleta matokeo ya haraka.


Pia amesisitiza TADB kutafuta fedha na mitaji ili kukuza mtaji wa benki pamoja na kuiga mfano kutoka katika nchi kama za India na China.

Post a Comment

HOME

 
Top